Image result for soda images without a copyright
Soda na vinywaji vingine vyenye kuongezwa sukari vimekuwa vikitumika kwa wingi kama sehemu ya mlo na kiburudisho. Vinywaji hivi huwa na sukari aina ya fructose au sucrose. Tafiti zimeonesha matumizi ya vinywaji hivi yamekuwa yakichangia kutokea kwa uzito wa kupindukia (obesity) na hatari ya magonjwa kama kisukari, magonjwa ya moyo na shinikizo la damu la kupanda.
Vinywaji hizi hasa soda huwa havina virutubisho vyovyote muhimu kwa mwili. Chupa ya soda ya mililita 330 huwa na sukari kiasi cha gramu 45 kwa wastani.
Soda na tatizo la uzito wa mwili.
Karibia asilimia 66 ya wamarekani wanatatizo la kuwa na unene na uzito wa kupindukia.Ripoti iliotolewa na Chuo cha Afya ya JAmii cha Harvard nchini marekanai, imeonesha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya unwaji na soda na ongezeko la uzito mwilini.Soda inachangia asimia saba ya wastani wa kalori zinazoingia miilini kwetu kwa kila siku.Kalori za kwenye soda zinaonekana nyepesi kulinganisha na kalori za kwenye chakula cha kawaida, kwa kuwa  chakula kitatufanya tushibe ila soda ni kimiminika, ambapo kalori zilizomo kwenye soda zitafyonzwa na kuingia katika mfumo wetu wa chakula pasi na kujisikia kushiba.Soda moja kwa siku yaweza changia ongezeko la hadi kilo 6.2 na mafuta mwilini kwa mwaka.
Soda na Magonjwa sugu
Soda ni sawa na dampo la sukari, iliyokatika mfumo wa fruktos.Kopo moja la soda ni sawa na vijiko vya chai  kumi vya sukari.Kitengo c ha Afya ya moyo marekani ili kuepusha madhara ya sukari kimeshauri mtu mzima kunywa chini ya vijiko sita vya sukari kwa siku, watoto visizidi vitatu, ila vijana walio wengi wanakunywa hadi vijiko 34 vya sukari kwa siku kutokana na kunywa vinywaji vitamu mara kwa mara.
Kubugia soda ya changia ongezeko la sukari kwenye damu, kwa kipindi fulani hii yaweza kuwa sababu ya maradhi kama kisukari, moyo, na pengine kansa.watafiti wakaendelea kusema asilimia 50 ya wanaotumia walau gramu 31 ya soda kila siku wana hatari ya kuugua maradhi ya dizaini hii, moja ya sababu inayoweza pelekea maradhi kwama stroku, kisukari na kusinyaa kwa mishipa ya damu.
Hii inaashiria ongezeko la unywaji wa soda kwa watu wazima itapelekea ongezeko la maradhaki haya katika miongo ijayo.
Soda na tatizo la mifupa
Tatizo jingine kwa vijana ni tatizo la afya ya mifupa, kama ilivyozoeleka kwa vijana na hasa watoto kupenda kunywa soda na vinywaji vitamu kwa wingi, na kunywa maziwa kwa uchache
Maziwa yana madini ya calcium, madini muhimu katika ukomavu wa mifupa, kama ilivyo kwa protini na virutubisho vingine vilivyomo kwenye maziwa.soda ina madini ya fosfeti., madini ambayo yanaweza athiri ujazo wa mifupa.  Iwapo itaingia mwilini kwa wingi kulinganisha na kiwango cha calcium. Tafiti zimethitisha kuna uhusiano wa karibu baina ya unywaji wa soda na tatizo la mifupa kwa wanawake watu wa wazima.
Soda na Kuoza kwa meno
Umakini umeelekezwa sana kwenye uhusiano wa soda na ongezeko la uzito mwilini. Uhusiano wa soda na athari zake kwa meno halijatazamiwa kwa kutosha.athari iliyopo haitokani tuu na sukari iliopo kwenye soda, bali hata kemikali zilizomo kwenye vinywaji vitamu, vya weza changia uharibifu wa meno kwa fujo.
Ni juu yetu kupima uzito wa maelezo haya katika kuamua kwamba soda inafaida kwetu au laa, ingawa zipo soda ambazo hazina sukari, Diebetic soda. Changamoto na uamuzi unabaki mikononi kwetu.
 
Top