Kuungua kwa watoto kwa moto ni moja ya ajali zinazotokea sana mara kwa mara na huwakuta wakiwa majumbani mwao. Asilimia 70 ya kuungua kwa watoto huwa ni wao wenyewe ndio hujitumbukiza katika ajali hizi pasipo kujijua au kudhamiria.

Watoto wako katika hatari ya kupata madhara mengi Zaidi wanapoungua kwa sababu bado wana miili midogo, ngozi ndogo na kinga ya mwili ambayo haijawa imara.

Hivyo pale wanapokuwa na majereha ya kuungua wapo katika hatari ya kupata maambukizo katika majeraha na kunyemelewa na maradhi mengine.

Ikumbukwe kuwa ngozi ndio ogani kubwa kuliko zingine mwilini, ikiundwa na tando kuu tatu. Ngozi ina kazi ya kukukinga na miale hatari ya jua, kuzuia maji yasipotee mwilini, kutoa uchafu mwilini, hutengeneza vitamin D, pia ni kama urembo wa kupendezesha mwili.

Mara nyingi watoto huunga kwa kugusana na kitu kilichopata moto kama pasi, maji yaliyochemka na kugusana ma mwale wa moto mkavu. Makali ya jeraha hutofautiana kulingana na ajali ya moto ambayo mtoto amepata. Ajali za kuungua moto zinatokea nyumbani mara nyingi majeraha yake huathiri Zaidi sehemu ya kwanza yay a ngozi nay a pili, huwa hayafiki katika msuli wa mfupa.

Mtoto kulia ni ishara ya maumivu makali, kuungua sehemu ya juu ya ngozi mahala ambapo huwa na mishipa mingi ya fahamu. Hii ndiyo sababu ya maumivu huwa makali kama sehemu ya kwanza ya ngozi huwa haitengenezi malenge lenge, sehemu ya pilui ya ngozi ndio huwa na malenge lenge.

Matatizo ambayo anaweza kuyapata mgonjwa aliegua ni kupoteza maji na chumvi mwilini. Kupata mshituko kutokana na maumivu makali,
 
Top