Uzazi wa mpango una mambo mengi sana.. sio kuzuia mimba tu ndio uzazi wa mpango ila hata kupanga idadi na jinsia za watoto ni moja ya njia za uzazi wa mpango..

Watu wengi wamekua wakitamani jinsia flani za watoto ili wazae watoto wachache ila kukosa kwa jinsia waliyoipanga hujikuta wakizaa watoto wengi wakati wakitafuta jinsia husika, mpaka familia hugombana na kutengana kwa sababu hizi.

Mara nyingi wazazi wa kiume hufikia hatua ya kuvunja ndoa kabisa hasa wanapokosa watoto wa kiume.

Leo ntamaliza kitendawili hiki kwa kutoa njia ambazo zinaweza kufanya mtu kupata mtoto wa kiume kwa asilimia nyingi…

Kitaalamu mbegu  zinazotoa mtoto wa kiume XY huenda kwa mwendo mkali sana kwenda kwenye mfuko wa uzazi lakini hufa haraka. lakini mbegu zinazotoa mtoto wa kike XX husafiri taratibu na huchelewa kufika na kufa  ndani ya mfuko wa uzazi kwani mbegu hizi huweza kuvumilia hali mbaya ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke, hivyo njia pekee ya kupata mtoto wa kiume ni kuhakikisha mbegu hizo za kiumeXY zinakutana na mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla ya kufa..

Zifuatazo ni njia hizo tano kali…
1. Hakikisha unashiriki tendo la ndoa siku mayai ya mwanamke yanapokua yameshuka{ovulation}
Ukishiriki tendo la ndoa siku hii ambayo yai linakua limeshuka    mbegu za kiume huweza kufika mapema na kujiunga na mayai ya kike  na kutengeneza mtoto{fertilization}hii ni siku ya 14 KABLA YA KUONA DAMU YA MWEZI UNAOFUATA SIO BAADA YA KUONA SIKU ZAKO..

Kama wewe mwanamke hujui siku yako ya ovulation fanya hivi.
Pima joto lako la mwili: nunua kipima joto[thermometer} na kisha pima joto lako kila asubuhi , siku ukiona joto lako limeongezeka kidogo ujue umeanza ovulation na hiyo ndio siku muhimu ya kutafuta mtoto..

Angalia maji maji ya uke: kawaida maji ya uke hua mazito na kuvutika kama maji ya mayai mabichi wakati mwanamke anapoanza ovulation..

2. Wewe mwanaume ongeza idadi ya mbegu zako..{sperm count}
Mwanaume anatakiwa aongeze wingi wa mbegu zake hasa kwa kukaa siku mbili mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa wakati akisubiri mwanamke wake aanze ovulation.

Njia zingine za kuongeza mbegu ni weka korodani kwenye hali ya ubaridi:
kawaida korodani hutengeneza mbegu nyingi wakati wa hali ya ubaridi kuliko joto  hivyo mwanaume anatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, na  kuwekalaptop kwenye mapaja acha kuvuta sigara na kunywa pombe:wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta sigara hua na mbegu kidogo sawasawa na wavutaji wa bangi.. matumizi ya dawa za cancer pia husababisha uzalishaji wa mbegu kidogo sana.

3. Tumia style za ngono ambazo zinahamasisha muingilio mkubwa{deep penetration}
Hii huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume{XY} kufika haraka na kufanya fertilization na upande mwingine, muingiliano mdogo{shallow penetration}husababisha mbegu kumwagwa mbali na mlango wa mfuko wa uzazi hivyo mbegu huweza kukutana na hali ya tindikali kwenye uke hivyo mbegu za mtoto wa kiume  kufa haraka na kuziacha mbegu zinazotoa mtoto wa kike.{XX}.

4. Hakikisha mwanamke anafika kileleni:
Mwanamke anapofika kileleni hutoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi wa tindikali ambayo ni adui wa mbegu  zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo hua haziwezi kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.

5. Usifanye tendo la ndoa kabla na baada ya ovulation;
Kabla ya ovulation mbegu za mtoto wa kiume XY hufika haraka kwenye mfuko wa uzazi  kama kawaida na kukuta mayai ya mwanamke hayajafika na kufa vivo hivyo baada ya ovulation..
 
Top