Tafiti mpya zinazidi kuonyesha namna mmea huu ulivyo wa mhimu kwa afya ya binadamu ikihusisha uwezo wake wa kudili na aina mbalimbali za kansa mwilini na tafiti nyingine zinaendelea kufanyika.
Tangawizi inaweza kuwekwa karibu kwenye kila chakula, iwe ni katika kuilainisha nyama nyekundu, kuongeza radha katika nyama au samaki, kama chai, kwenye juisi na kadharika. Binafsi napenda ikiwa kwenye juisi ya matunda ndiyo inakuwa tamu zaidi na inaenda kufanya kazi mwilini haraka zaidi.
Tangawizi ni zao la kibiashara na ni rahisi kutoka kimaisha kama utaamua kulima tangawizi ingawa ni zao la miezi mingi lakini ukivumilia utakula bata tu, gunia moja linauzwa kati ya laki 3 hadi 6 wakati wa msimu mzuri.
Tangawizi iliorodheshwa kwa mara ya kwanza na serikali ya Marekani kama dawa kwa ajili ya binadamu kati ya mwaka 1820 na 1873.
Tangawizi huongezwa pia katika vinywaji vingi vya viwandani zikiwemo soda ili kupata radha nzuri zaidi.
Leo nimekuletea hii juisi ya tangawizi, nimetumia tangawizi mbichi za ukubwa wa kati nne, parachichi moja na asali mbichi vijiko vikubwa saba na na maji lita moja na nusu.
Kazi 48 za tangawizi mwilini
- Huondoa sumu mwilini haraka sana
- Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi
- Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi
- Huondoa uvimbe mwilini
- Huondoa msongamano mapafuni
- Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake
- Huondoa maumivu ya koo
- Huua virusi wa homa
- Huondoa maumivu mbalimbali mwilini
- Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)
- Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.
- Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”
- Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-related cancer)
- Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)
- Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)
- Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo
- Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi
- Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi
- Huongeza msukumo wa damu
- Husaidia kuzuia shambulio la moyo
- Huzuia damu kuganda
- Hushusha kolesto
- Husafisha damu
- Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa
- Hutibu shinikizo la juu la damu
- Husafisha utumbo mpana
- Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma
- Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI
- Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
- Dawa nzuri ya kuondoa uchovu
- Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu
- Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa
- Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula
- Husaidia kuzuia kuharisha
- Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu
- Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto
- Hutibu homa ya kichwa
- Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
- Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito
- Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)
- Huimarisha afya ya figo
- Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi
- Ina madini ya potassium ya kutosha
- Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.
- Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha
- Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium
- Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene
- Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita