mimba 4
Tukizungumzia afya ya wanawake na matatizo yanayoikumba basi hatuwezi kuacha kuzungumzia tatizo hili hata sekunde moja. Ni moja kati ya matatizo yanayowakumba wanawake wengi walio katika umri mbalimbali (Chini ya miaka 35, miaka 35 na zaidi ya miaka 35) na kuwanyima raha na amani ya maisha. Akina mama wengi wamejikuta hawana raha na ndoa na maisha yao kwa ujumla na wengine wametumia au wanatumia pesa nyingi kuhangaika kutatua tatizo hili.
AFYA ZAIDI CONSULTANTS tupo pamoja na wanawake wote na tunapenda kuwasaidia na kuwaombea ili waweze kuwa na afya njema, furaha na amani katika maisha yao yote.
Kupata mimba kuna husisha mambo mbalimbali ambayo yanaangukia katika makundi makuu mawili :
  1. Muundo wa mwili na sehemu zinazohusika na uzazi
  2. Ufanyaji kazi wa mwili na sehemu zinazohusika na uzazi
Kitu chochote kitakachoharibu muundo na ufanyaji kazi wa mwili na sehemu zinazohusika na uzazi huweza kusababisha mwanamke husika kushindwa kushika mimba.
Tafiti nyingi zimefanyika na kupata sababu zifuatazo  kuwa zinaweza kusababisha au kuchangia mwanamke kushindwa kupata mimba:
SABABU YA KWANZA : KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI (FALLOPIAN TUBES)
Sababu hii huchangia kwa 30% ya wanawake wote wanaoshindwa kushika mimba. (Katika kila wanawake 10 wanaoshindwa kupata mimba, zaidi ya watatu hushindwa kwa sababu hii).
Mirija hii ndiyo hutumika na mbegu za kiume kupita kwenda zilizo mbegu za kike kuungana na kusababisha mimba. Kuziba kwa mirija hii hupelekea mbegu za kiume kushindwa kupita na kwenda kukutana na mbegu za kike, hivyo hakuna mimba itakayotungwa.
SABABU YA PILI : UPUNGUFU WA MADINI YA CHUMA/DAMU
Tafiti zinaonesha kwamba wanawake wenye upungufu wa madini ya chuma hukabiliwa na changamoto katika uzalishaji wa mayai (mbegu za kike) na hata yakizalishwa huwa na afya duni. Hii hupelekea asilimia 60 ya wanawake hawa (Wanawake 6 kati ya 10) kushindwa kushika mimba ukilinganisha na wale wasio na upungufu wa madini ya chuma/damu
SABABU YA TATU : MATATIZO KATIKA MBEGU ZA KIUME AU MWANAUME MWEYEWE
Kwa miaka mingi hili lilikuwa halijulikani au halitiliwi maanani, na macho yote yalikuwa kwa mwanamke. Lakini sasa tafiti zimebaini kwamba afya duni ya mwanaume au mbegu za kiume, idadi ndogo na kukosa uwezo mzuri wa kuogelea na kwenda kufuata mayai ya kike huchangia tatizo la wanawake kushindwa kupata mimba kwa 20% (1 kati ya ndoa 5 zinazoshindwa kupata mtoto). mimba 1
PICHA : Mbegu za kiume (Nyeupe/Bluu) zikiwa zinaogelea kulikimbilia yai (Mbegu ya kike)


SABABU YA NNE : ULAJI MBAYA NA UKOSEFU WA CHAKULA BORA (MILO KAMILI)
Mtindo mbaya wa maisha hususan katika lishe na ulaji huchangia pia tatizo la kushindwa kupata mimba. Hii ni kwa sababu ukosefu wa chakula bora na ulaji mbaya hupelekea kukosekana kwa virutubisho muhimu kwa ajili ya ufanyaji kazi wa mwili na mfumo wa uzazi. Pia huweza kumpelekea mwanamke kuwa na magonjwa na matatizo mengine ambayo yanaweza kuingilia uzazi.
SABABU YA TANO : MSONGO (STRESS) AU MATATIZO KATIKA HOMONI
Uzazi na maisha yetu kwa ujumla huratibiwa na vitu vinavyoitwa homoni. Homoni hutoa ishara na kufanya sehemu mbalimbali za miili yetu kufanya kazi au kuacha kulingana na mahitaji. Kwenye uzazi tuna homoni pia, mifano ni OestrogenProgesteroneLuteinizing hormone na Oxytocin. Matatizo yoyote katika uzalishwaji au utendaji kazi wa homoni za uzazi huweza kupelekea matatizo katika uzazi, moja wapo ikiwa ni kushindwa kupata mimba.
Msongo huweza kuvuruga uzalishwaji au ufanyaji kazi wa homoni na hivyo kuathiri uzazi kwa ujumla. Huweza kupelekea hata mimba ambayo imeshatungwa tayari kuweza kutoka na kuharibika
SABABU YA SITA : KUSHINDWA KUZALISHA MAYAI (MBEGU ZA KIKE)
Inatokea pia kutokana na matatizo katika homoni au ovari (Sehemu ya uzazi ya mwanamke inayofanya kazi ya kuzalisha mayai/mbegu za kike). Matokeo yake ni kwamba mbegu za kiume zitakosa mbegu za kike za kuungana nayo na kutengeneza mimba, hivyo mimba haitatungwa.mimba 3
SABABU YA SABA : MBEGU ZA KIUME KUSHINDWA KUPITA KWENYE SHINGO YA UZAZI/UKE (CERVIX) NA KWENDA KWENYE MJI WA MIMBA NA MIRIJA YA UZAZI
Matokeo ya hii ni mbegu za kiume kushindwa kuzifikia mbegu za kike, hivyo mimba haitatungwa. Hata kama kila kitu kipo sawa kwa mwanamke na mwanaume dosari hii inaweza kupelekea mwanamke kushindwa kupata mimba. Pia inaweza ikatokea mbegu za kiume zikawa zinakufa hapa kutokana na ukali wa asidi katika sehemu za uzazi za mwanamke.
SABABU YA NANE : UWEPO WA MAJERAHA, MAKOVU, UVIMBE, VITU VIGENI NA MATATIZO MENGINE KATIKA MAENEO AMBAYO MAYAI YA KIKE HUZALISHWA, MIMBA HUTUNGWA NA MIMBA HUKAA HADI KUJIFUNGUA
Hapa ndipo wanawake wenye uvimbe na vitu vingine (CystsFibroids, Endometriosis, Pelvic Inflammatory Disease/PID) kwenye tumbo la uzazi huangukia. Majeraha na makovu (kwa mfano yanayotokana na utoaji mimba) huweza kusababisha mwanamke kushindwa kushika mimba pia.
SABABU ZINGINE
Sababu zingine huweza kwa namna moja au nyingine  kuchangia (Kwa kiasi kidogo) tatizo la kushindwa kushika mimba (Kemikali, magonjwa, hitilafu katika kinga ya mwili nk)
Mifano ni simanzi (depression),  vilainishi vinavyotumika wakati wa kujamiiana, uvutaji sigara na bangi, unywaji pombe, madawa ya kulevya, uzito mkubwa/mdogo (wembamba) na uliopitiliza, uchafuzi wa mazingira, hitilafu katika kinga ya mwili na kuharibu mbegu za uzazi na ujauzito, kukosa usingizi wa kutosha na kadhalika.
Hizo ndizo sababu kuu na sababu nyingine zinazoweza kusababisha au kuchangia tatizo la mwanamke kushindwa kushika mimba. Ni muhimu kupata ushauri na vipimo kwa wataalam, hususan hospitali, ili kuweza kujua chanzo cha tatizo na kuanza kutibu.
mimba
Kwa wanandoa au mwanamke na mwanaume waliopo pamoja ni vyema wakahusika wote kwa pamoja kufanyiwa uchunguzi na kutafuta tiba ya tatizo lao na sio mwanamke peke yake.
Sasa hivi teknolojia imeendelea na sababu zote hapo juu huweza kutibiwa na mwanamke kuweza kupata mimba bila tatizo. Cha msingi ni kufuatilia na kujua chanzo kisha kutafuta matibabu yake sahihi.mimba 5
Kushindwa kupata mimba ni tatizo linaloweza kutibika kwa asilimia 100% !
Tuna uhakika na hilo na tunajua linawezekana. Pata ushauri, uchunguzi na matibabu mazuri tu.
AFYA ZAIDI CONSULTANTS tupo pamoja na wanawake wote na tunapenda kuwasaidia na kuwaombea ili waweze kuwa na afya njema, furaha na amani katika maisha yao yote. Tunakutakia afya njema!
 Kwa ushauri binafsi na maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa
Simu : 0625539100
 
Top