urembo 3 Kila mtu anapenda kuwa na ngozi nzuri inayopendeza. Hakuna anayependa kuwa na ngozi yenye makunyanzi, chunusi, michirizi, mafuta mengi, harufu mbaya, madoadoa, makovu, vipele wala ngozi kavu. Wengi wetu tunatumia vipodozi kwa sababu kuu mbili
  1. Kuondoa matatizo mbalimbali kwenye ngozi
  2. Kuipendezesha ngozi na kuifanya ivutie
Tunatumia vipodozi vya aina mbalimbali na gharama tofauti. Umewahi kujiuliza tofauti kati ya losheni au mafuta au krimu za aina mbalimbali ni ipi?
Umewahi kujiuliza tofauti kubwa ya bei kati ya vipodozi vya aina mbalimbali inatokana na nini?
Umewahi kujiuliza ngozi inahitaji kutunzwa na kupendezeshwa vipi ili iweze kuwa nzuri na ya kuvutia?urembo
Jibu hayo maswali vizuri sana kisha utajua namna ya kuokoa pesa ambayo ungetumia katika vipodozi visivyokufaa kwa ngozi na mahitaji yako.
JINSI YA KUIPENDEZESHA NGOZI YAKO
Ngozi zetu zinajitengeneza na kujikarabati zenyewe kila siku. Zinafanya hivyo kwa kutumia virutubisho (Vitamini, Madini, Mafuta na Protini) ambavyo tunakula kupitia vyakula vyetu. Pia ngozi zetu zinatumia maji kujizuia zisikauke na kunyauka.
Vitamini A, B, C na E ni muhimu sana kwa ngozi na nywele zetu. Madini ya Potasiamu, Seleniamu, Zinki, Chuma, Madini ya joto (Iodine), kalsiamu, kobalti nk.
Hivyo vyote ni muhimu sana kwa ngozi zetu na upungufu wake ndio husababisha ngozi kuwa kavu na kunyauka na kuanza kuzeeka.
Kwa kifupi, Chakula bora na Mlo kamili ndio nguzo ya kwanza ya ngozi nzuri inayopendeza.
Matatizo mengi katika ngozi zetu yanatokana na lishe mbovu na ulaji mbaya. Pia kutokunywa maji ya kutosha.
Kula sana mboga za majani na matunda na kunywa sana maji ili upate virutubisho muhimu kwa ngozi yako na ngozi yako itakuwa vizuri kila siku.
Cha pili ni Usafi. Fanya usafi wa kutosha kwenye ngozi yako kila siku. Osha ngozi vizuri na oga kwa urembo 2sabuni zinazosaidia kuondoa vijidudu kama vile bakteria, jasho lote, vumbi na mafuta ya ziada kwenye ngozi yako. Hakikisha sabuni yako ina ufanisi mkubwa wa kuondoa uchafu na vijidudu, vinginevyo uchafu utakuwa unajirundika siku hadi siku na ngozi yako itakuwa inafubaa japokuwa unaoga na kuisafisha. Hapa tunakushauri utumia Shower gel au Face wash/Facial cleanser au sabuni za Protex, Dettol , Pears na nyinginezo zenye dawa na uwezo mkubwa wa kuondoa uchafu na vijidudu vingi.
Cha tatu ni vipodozi salama na vinavyoendana na ngozi yako. Anza kujua ngozi yako ni ya aina gani (Ya kawaida, kavu, ya mafuta au mchanganyiko) kisha tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako. Hata losheni ya shilling Elfu Nne tu (4,000/=) inatosha kabisa kuipendezesha ngozi yako endapo utazingatia Vyakula bora, Milo kamili na Usafi mzuri wa ngozi yako kila siku.
Watu wengi hudhani na kuamini kwamba losheni za bei kubwa ndizo nzuri kwao na hivyo kuzinunua na kuanza kuzitumia. Baada ya muda hawapati matokeo waliyoyataka au hupata matokeo ya tofauti na kuamua kuacha na kununua ya aina nyingine na nyingine na nyingine.
Hilo ni kosa kubwa sana. Na ndilo kosa linalowapotezea watu wengi pesa zao, muda wao na uzuri wao.
Tunza ngozi yako vizuri kwa chakula bora, mlo kamili, kunywa maji ya kutosha na fanya usafi mzuri sana.
Cha nne ni kuepuka vipodozi visivyo salama. Kwa kiasi kikubwa watu wengi hupata matatizo kama vile chunusi, madoadoa, makovu, michirizi, ngozi kuwa na rangi mbalimbali na zisizopendeza, ngozi kuungua, weusi kuzunguka macho nk kutokana na matumizi ya vipodozi visivyo salama. Matokeo yake ni kupoteza pesa nyingine tena kubwa zaidi kuanza kutibu matatizo hayo. Kama hutaki kupoteza pesa nyingi kwenye vipodozi basi epuka kabisa vipodozi visivyo salama. Acha kabisa vipodozi visivyo salama. Hata kama siku za kwanza vinaleta matokeo mazuri kiasi gani, baadae vinaleta matatizo makubwa sana na yanayogharimu oesa nyingi, afya na maisha yako kwa ujumla.
Cha tano ni kuepuka jua kali. Unaweza ukawa unajipendezesha vizuri lakini ukiwa unapigwa na jua kali basi jua linaharibu ngozi yako na kupoteza thamani ya vipodozi vyote. Jua kali huharibu ngozi zetu na kwenda kinyume na malengo yetu ya kupendezesha ngozi. Unaweza ukaepuka jua kali kwa kushinda na kufanyia kazi zako kivulini, kuvaa nguo zinazofunika mwili wako vizuri au kupaka vipodozi vinavyoukinga mwili wako dhidi ya jua (Sun screens / Sun blockers).
Hautahitaji tena vipodozi vya bei mbaya ili kuondoa madhara yanayoletwa na jua katika ngozi yako. Kinga ni bora kuliko tiba.
  Cha sita ni kuondoa seli za ngozi zilizokufa (Exfoliation) ambazo
urembo 4 husababisha ngozi kufubaa na kuzeeka.  Hakikisha unatumia njia salama kabisa kama vile Scrub na inayoendana na ngozi yako. Fanya hivyo mara moja hadi mbili kwa wiki. Usitumie isiyoendana na ngozi yako maana itakuletea chunusi na kukuharibia ngozi yako.
   HITIMISHO
Umeona? Ni rahisi kama hivyo. Ukizingatia hayo hautadanganyika tena kutumia vipodozi vya bei kubwa ambavyo kazi zake na ufanisi wake ni sawa tu na ule wa vipodozi vya bei ndogo. Cha msingi ni kuitunza ngozi yako vizuri na kutumia vipodozi salama na vinavyoendana na ngozi yako.
Usipoteze tena pesa zako na wala usiharibu ngozi yako. Unaweza kupendeza na kuwa na ngozi nzuri kila siku bila kutumia gharama kubwa. Anza sasa. Fanya hivyo kila siku.
Unaweza kujifunza zaidi haya na mengine mengi kwenye kitabu cha SURA NZURI NGOZI NYORORO. Tumeelezea vizuri sana kuhusu ngozi na maisha yake. Tumeelezea jinsi ya kuitunza na kuipendezesha ngozi vizuri.
Pendeza bila gharama. Pendeza bila kujidhuru.
Kwa maelezo zaidi na ushauri binafsi unaweza kuwasiliana nasi
MAWASILIANO : 0625539100
 
Top