Kama umekonda na kudhoofika mwili kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuugua magonjwa na maradhi mbalimbali au kupatwa na msongo mawazo, basi fuata maelekezo yafuatayo ili upate kujua namna ya kuandaa na kutayarishe lishe maalumu ya asili itakayo kusaidia kunenepa na kurejesha afya ya mwili wako katika hali yake ya kawaida.
MAHITAJI:
1. Dawa Lishe ya kuongeza na kunenepesha mwili
2. Asali ya tende
3. Ufuta
4. Ukwaju
5. Kitunguu swaumu
6. Giligiliani
7. Juisi ya Komamanga na Asali
MATAYARISHO NA MATUMIZI
Matumizi ya lishe hii, yame gawanyika katika awamu kuu mbili. Awamu ya kwanza, itachukua siku thelathini na awamu ya pili itachukua siku thelathini pia.
Katika awamu ya kwanza , mgonjwa atatumia DAWA LISHE YA KUNENEPESHA MWILI, ASALI YA TENDE NA UFUTA na awamu ya pili, mgonjwa atatumia UKWAJU, KITUNGUU SWAUMU, GILIGILIANI na JUISI YA KOMAMANGA & ASALI kwa kufuata utaratibu utakao elezwa hapo chini.
AWAMU YA KWANZA
SIKU THELATHINI ZA KWANZA
Mahitaji
1. Dawa lishe ya kuongeza na kunenepesha mwili
2. Ufuta
3. Asali ya Tende ( Dates Syrup )
MATAYARISHO , MAELEKEZO NA MATUMIZI
1. Dawa –Lishe ya Kunenepesha Mwili
Chukua vijiko vitatu vikubwa vyenye dawa yako, kisha changanya na maji nusu lita halafu chemsha hadi itokote, Ikiisha tokota, ipua acha ipoe kidogo kisha tumia kunywa pamoja na machicha yake. Utafanya hivyo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa muda wa siku thelathini.
2. Ufuta : Matayarisho : Chukua vijiko vikubwa vinane vyenye ufuta, kisha changanya na lita moja na nusu ya maji. Kama hauna tatizo na sukari, unaweza kuongeza na sukari kiasi ili kuipa ladha. Ikisha tokota, ipua iache ipoe kiasi kisha tumia kula ufuta wote pamoja na supu yake ama juisi yake. Utafanya hivyo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa muda wa siku thelathini.
(N.B: KAMA UNA NAFASI, BADALA YA KUTUMIA VIJIKO VINANE TU VYA UFUTA KWENYE LITA MOJA NA NUSU YA MAJI, WEWE TUMIA ROBO KILO YA UFUTA KWENYE LITA TATU YA MAJI, CHEMSHA HADI ITOKOTE, IACHE IPOE, KISHA TUMIA KULA . FANYA HIVYO MARA MBILI KWA SIKU ASUBUHI NA JIONI KWA MUDA WA SIKU THELATHINI )
2. ASALI YA TENDE
3. Tumia kula vijiko vikubwa vinne vya tende mara mbili kwa siku asubuhi na usiku kwa muda wa siku thelathini. Yaani asubuhi kula vijiko vikubwa vinne na usiku kula vijiko vikubwa vinne vya asali ya tende.
AWAMU YA PILI
Awamu ya pili ya lishe hii, itaanza baada ya kukamilika kwa siku thelathini za kutumia dawa lishe, ufuta pamoja na asali ya tende. Kama ilivyo kuwa kwa awamu ya kwanza, awamu ya pili pia itachukua muda wa siku thelathini
MAHITAJI, MATAYARISHO NA MATUMIZI
1. UKWAJU
Matayarisho na Maandalizi
Chukua ukwaju kiasi cha robo kilo , weka kwenye maji kiasi cha lita moja, ongeza pilipili manga kiasi cha kijiko kimoja kidogo ( tea spoon ) halafu ongeza sukari vijiko vitatu vikubwa, ongeza karafuu ya unga kijiko kimoja kidogo, pamoja na hiriki vijiko vikubwa viwili.
Ukisha fanya hivyo, chemsha hadi mchanganyiko wako utokote. Ukisha tokota, ipua na kuchuja kisha weka kwenye chombo kisafi.
MATUMIZI :
Tumia kunywa mchanganyiko huu kila siku asubuhi baada ya kunywa chai. Utafanya hivyo kwa muda wa siku thelathini mfululizo.
2. JUISI YA KOMAMANGA NA ASALI
Matayarisho na Matumizi
Tayarisha juisi ya komamanga kiasi cha nusu lita, changanya na asali ya kawaida vijiko vikubwa vinane, kisha ongeza chumvi kijiko kidogo( tea spoon)
Koroga mchanganyiko wako halafu tumia kunywa. Utafanya hivyo mara moja kwa siku kwa muda wa siku thelathini.
Matunda ya makomamanga yanapatikana masokoni, ingawa mara nyingi hupatikana kwa uchache. Kama utabahatika kupata matunda mengi, basi unashauriwa kuyachukua kwa wingi na kuyahifadhi, sehemu salama ili usipate usumbufu wakati wa kutumia tiba yako.
Mbali na kutumika katika lishe ya kuongeza na kunenepesha mwili, tunda la komamanga, linasaidia kuondoa harufu mbaya ya kinywa. Kwa kuondoa harufu mbaya ya kinywa, kula walau tunda moja la komamanga kwa siku kwa muda wa siku thelathini mfululizo. Utapata matokeo mazuri . ( HII ITAWASAIDIA ZAIDI WALE AMBAO TATIZO LAO LA KUTOKWA NA HARUFU MBAYA YA KINYWA LIMEANZIA KINYWANI NA SIO TUMBONI
ALTERNATIVE (MBADALA ) WA JUISI YA KOMAMANGA ILIYO UNGWA NA ASALI.
Kama utashindwa kupata makoma manga, basi utafanya kama ifuatavyo :
KITUNGUU SWAUMU
Chukua punje nne za vitunguu swaumu, zitwange kisha tia kwenye maji nusu lita halafu ongeza juisi ya ndimu moja au limao moja kisha chemsha hadi mchanganyiko wako uchemke.
Matumizi : Tumia hivyo kila siku usiku baada ya kula chakula cha usiku. Utafanya hivyo kwa muda wa siku thelathini mfululizo.
AU
Vile vile , mbadala mwingine wa kutumia juisi ya komamanga iliyo changanywa na asali, unaweza kutumia JUISI YA GILIGILIANI kwa kufuata utaratibu ufuatao :
JUISI YA GILIGILIANI
MATAYARISHO NA MATUMIZI YA JUISI YA GILI GILIANI
Chukua giligiliani fresh, kisha zi -blend ( ZISAGE ) ili kupata juice yake kiasi cha robo lita.
Ndani ya juisi yako ya giligiliani, kamuliamo ndimu fresh moja, halafu ongeza chumvi kiasi robo kijiko kidogo ( tea spoon), koroga kisha tumia kunywa. Utakunywa usiku baada ya kula chakula cha usiku. Utafanya hivyo mara moja kwa siku kwa muda wa siku thelathini mfululizo.
PIA : Jenga utaratibu wa kuwa unakula giligiliani kwa wingi. Hakikisha katika kila mlo wako, inakuwepo mboga ya giligiliani pembeni.
VITU VINGINE VYA KUZINGATIA..
Pamoja na kutumia lishe hii ya asili kwa kufuata utaratibu huo hapo juu, unashauriwa kuzingatia matumizi ya vyakula vifuatavyo:
TANGAWIZI
Jenga tabia ya kuwa una tumia tangawizi, kila mara upatapo nafasi. Utaratibu wa jinsi ya kutayarisha tangawizi ni kama ifuatavyo :
Chukua kipande kimoja cha tangawizi, kisha kitwange halafu ongeza vikombe viwili vya maji vyenye ujazo wa milimita mia mbili na hamsini ( 250 mills). Chemsha pamoja kisha ongeza maziwa kiasi cha robo lita na sukari ili kupata ladha. Fanya hivi kila mara uapatapo nafasi. Ukiweza kufanya hivyo walau mara mbili kwa siku, itakuwa vizuri zaidi.
AU chukua kipande kimoja cha tangawizi, kitwange kisha chemsha pamoja na chumvi nusu kijiko kidogo kwenye maji kiasi cha nusu lita halafu tumia kunywa kikombe kimoja nusu saa kabla ya kula chakula chako cha asubuhi, mchana na usiku.
HIRIKI
Jenga utaratibu wa kuwa unakunywa mara kwa mara chai iliyo changanywa na hiriki.
MACHUNGWA
Jenga utaratibu wa kuwa unakula machungwa kwa wingi, kwa kadri utakavyo weza. Unashauriwa kuwa unachanganya na chumvi kidogo pamoja na pilipili manga.