BAADHI ya watu wamekuwa wakidai tunda la nanasi kuwa siyo salama kwa akina mama wajawazito, ingawa suala hili bado halijathibitishwa kitaalamu, kwani wapo wanaokula na haijawahi kuripotiwa madhara. Linatumika kama tunda ama juisi na lina faida mbalimbali kwa afya ya mwanadamu.
BAADHI YA FAIDA HIZO NI PAMOJA NA:
Lina vitamini A, B na C, madini ya chuma, calcium, copper na phosphorous ambayo yote ni muhimu sana katika afya ya mwanadamu.Tunda hili husaidia kutengeneza damu, kuimarisha mifupa , meno, neva na misuli (muscles).
Hutibu matatizo ya tumbo, bandama na ini, husaidia kusafisha utumbo mwembamba, hutibu homa, vidonda mdomoni, magonjwa ya koo, hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu, hutibu kikohozi, kutetemeka na uoga (Anxiety). Leo nimeandika tiba ya nanasi kwa sababu ni mjadala mkubwa ulioibuka kuwa tunda hili lina madhara, lakini nikuhakikishie msomaji hakuna madhara ya kukufanya