Nchini
Uturuki nilikuta kila asubuhi katika hoteli fulani wakati wa kifungua
kinywa kunakuwa na matunda ambayo kule kwetu milimani tunayaita thambia/sambia. Bahati mbaya sikuuliza yanaitwaje kwa Kiingereza. Ila niliyapiga picha na kuwaonyesha wanafesibuku kutoka huko kwetu na wakathibitisha
kuwa kweli ni hayo matunda. Jana bahati nzuri nilimuuliza dada wa
Kituruki hapa nilipo haya matunda wanayaitaje. Akasema wanayaita malta eriği (maltese plum) au muşmula, pia akasema wengine wanasema ni matunda kutoka 'dunia mpya' ('new world'). Ila akanipa linki hii hapa chini inayoonesha kuwa jina lake lingine ni Loquat na ni dawa. Sijui watu wa kule kwetu wanalitambua hilo au wanayala tu kama matunda pori mengine. Nitakapomtembelea Bibi yangu hivi karibuni nitamuuliza.