Familia zinazotumia maziwa ya kopo aina ya Lactogen,ambayo
yamesajili hapa nchini kwa ajili ya kutumiwa na watoto wachanga,zina
hali ngumu baada ya kuadimika,huku ikielezwa kuwa yatazidi kuadimika kwa
zaidi ya miezi miwili ijayo.
Uchunguzi umebaini kuadimika kwa maziwa hayo yanayotengenezwa nchini
Ufaransa kunafanya baadhi ya familia kununua kwa bei kubwa na wengine
kulazimika kubadili aina ya maziwa kwa watoto wao.
Mmoja wa wauzaji wa maziwa hayo kwa rejareja alisema tatizo hilo
lilianza kujitokeza mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka jana na kufanya bei
yake kupanda kutoka 15,000 kwa kopo hadi 20,000.
Kwa upande wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA
kupitia Ofisa habari wake Gaudensia Simwanza mamlaka yake inasimamia
ubora wa bidhaa za maziwa ya watoto na wamekua wakiendesha operesheni ya
kuondoa bidhaa hizo feki.