
Hilo ndilo la jambo la msingi kwa sasa na kila
familia inatakiwa kulizungumza jambo hili kwa kina huku taarifa sahihi
zikitumika zaidi.Hii ni nafasi nzuri kwani itasaidia kujikinga mapema kabla ugonjwa huu haujafika katika
ngazi za familia na nchi.
Wakati wote tumekuwa tukishauriwa
na wataalamu wa Afya kunawa mikono kwa kufuata kanuni lakini wangapi wanafanya
hivyo na wangapi wanasimamia hilo katika ngazi za familia bado ni changamoto
lakini bado watalamu wanaendelea kushauri na kusisitiza kuwa kufuata kananu za
unawaji mikono ni namna nzuri ya kujikinga na magonjwa hasa nykati hizi ambzo
Ebola imekuwa tishio kwa dunia nzima.Huu ni wakati ambao katika kila ngazi ya
familia lazima kanuni hizi za unawaji mikono zifuatwe kwa mfano na sio maneno.
Katika ngazi za familia wazazi
hujadili kuhusu maadili zaidi hasa ya mavazi na adabu lakini hizi ni nyakati za
kuanzisha mtindo mpya wa kuwa siliana kwa kina kuhusu Ebola .Wengi mtakuwa
mashahidi jinsi ilivyo kuwa changamoto kujadili kuhusu Ukimwi na hata maswala
ya kiafya katika ngazi za famila.Nyakati hizo zimepitwa tusije kufanya makosa
tena ni jukumu la familia kuwa na taarifa sahihi kuhu Ebola na maswala mengine
ya kiafya maana hali si nzuri kwa wenzetu ndio maana wasahili wakasema ukiona
mwenzio ananyolewa basi wewe tia maji.
Ukiwa mjini hata vijini watu hupenda
kusalimiana kwa kupeana mikono ila wakati huu lazima tujifunze usatarabu mpya
na kanuni za kiafya ili kujikinga na Ebola huu ni wakati wa kufuata usatarabu
na kuzingatia kanuni za afya.
Tusikubali kuwa na utamaduni wa kujua wangapi
wamekufa au wangapi wame ambukizwa tuu hii pekee yake haitoshi tubadili mtazamo
wangapi wamejikinga na kubadili mwenendo ili na sisi tuweze kujifunza kanuni ili
tujikinge.
Tusikubali kujua neno Ebola pekee yake wakati nafasi na fursa ya kujifunza
kupitia mitandao ni pana.Vijana na jamii ni lazima kuzinduka ili tutafute
taarifa kuhusu Ebola ili tuweze kufanya uamuzi sahihi na kujikinga.
Ni ugwana kutumia vifushi ulicho jiunga hii leo kutafuta taarifa sahihi
kuhusu Ebola na kujenga mazoea ya kujua usatarbu na kanuni za kiafya maana
waswahili husema bora kinga kuliko tiba.
Taarifa inayo patikana katika tovuti ya Al-Jazeera
zinaonyesha kuwa asiliia 70 ya watu wanaoambukizwa Ebola hufaliki [1]
huku gazeti la Daily news lenye kichwa cha habari (Ebola orphans in west Africa
face stigma) likiwa na taarifa
linaonyesha njinsi gani ugonjwa huu
unazidi kuathiri maisha ya familia katika bara la Afrika na watoto wakibaki
yatima.
Hatuna namna zaidi ya kubadili ustarabu
na kufuata kanuni za kiafya ili kujikomboa.Katika ngazi za familia lazima
jukumu hili la kujikinga na kuzungumza kuhusu afya liwe endelevu na kwa mifano.