Kama utakuwa upo karibu sana na mitandao ya kijamii ya Mandai Herbalist Clinic basi naamini utakuwa unakumbuka kuwa Jumapili ya juzi ya Agosti 23, 2015 Tabibu Abdallah Mandai alionekana Star Tv kupitia kipindi cha Mandai afya.com akizungumzia kuhusu nanasi.

Kufuatia kipindi hicho kumekuwa na maswali mengi wengi wakihitaji kujua umuhimu na faida za tunda hilo la nanasi.

Hivyo bila hiyana nimeona ni vyema nikupe hii orodha ya faida za nanasi kwa ujumla wake kama ifuatavyo:

Mizizi ya nanasi inapochemshwa huwa ni dawa ya matatizo ya figo na kuua minyoo mwilini.

Juisi ya majani yake ni dawa ya kutibu vidonda na matatizo ya magonjwa ya ngozi na majipu.

Maua ya nanasi yanapochanganywa na asali huwa ni tiba ya mafua na kikohozi, tumia kijiko kimoja kwa siku.

Nanasi pia huwa ni msaada kwa wale wenye shida ya matatizo ya akili na kupoteza kumbukumbu.

Tunda hili pia husaidia kutibu matatizo ya tumbo, ini, magonjwa ya bandama, homa, pumu pamoja na kusaidia kuongeza maziwa kwa kinama.
 
Top