Saratani ya shingo ya kizazi ni tatizo hatari linaloweza kusababisha kifo ambalo husababishwa na virusi viitwavyo 'Human Papilloma Virus' (HPV)

Zifuatazo ni sababu ambazo huweza kumuweka mwanamke katika hatari ya kukubwa na saratani ya shingo ya kizazi.

Kujihusisha na ngono wakati wa umri mdogo
Wasichana wanaoanza kujamiana wakiwa na umri mdogo wako katika hatari ya kupata saratani hii ya shingo ya kizazi. Hivyo ni vyema kuepuka kujihusisha na ngono ukiwa na umri mdogo.

Kuwa na mahusiano na wapenzi wengi
Mwanamke mwenye wapenzi wengi au mwenye mwanaume ambaye anawapenzi wengi yote hayo huchangia kumuweka mwanamke katika hatari kubwa ya kupata saratani ya shingo ya kizazi .

Kujifungu watoto wengi.
Wale kinamama ambao hujifungua watoto wengi, huweza kuwa katika hatari ya kukubwa na tatizo hili la saratani ya shingo ya kizazi, ndio maana baadhi ya wataalam wamekuwa wakishauri angalau mama anapofikisha watoto watano akasitisha zoezi la kuendelea kuzaa.

Historia ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia.
Aina hii ya saratani pia huhusishwa sana na masuala ya kurithishwa katika familia ya mgonjwa husika.

Upungufu wa kinga za mwilini
Magonjwa yanayosababisha upungufu wa kinga mwilini kama Ukimwi huweza kuchangia mhusika kupata saratani hii kwa urahisi zaidi .

Mbali na sababu hizo dalili au viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi ni pamoja na kutokwa damu katika tupu ya mwanamke (uke) ambayo si ya kawaida inaweza kuwa matone au damu inayotoka katikati ya mzunguko wa hedhi (yaani baada ya hedhi au kabla ya hedhi inayofuata).

Dalili nyingine ni kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa, lakini pia unaweza kupata maumivu makali wakati wa kujamiana.
 
Top