Ugonjwa wa kipindupindu kwa mkoa wa Dar es Salaam ulianza katika manispaa ya Kinondoni kuanzia Agosti 15 mwaka huu, na hadi sasa Manispaa tatu zimeathirika kwa ugonjwa huu.

Kwa upande wa Mkoa wa Morogoro ugonjwa huu ulianza tarehe 17 mwezi wa nane mwaka huu 2015

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Dk, Seif Rashid alizungumza na wanahabari za kuzitaja kanuni za afya ambazo kama hazitazingatiwa hupelekea kupata ugonjwa wa kipindupindu.

Hizi ndio sababu ambazo Dk. Seif Rashid alizitaja ambazo huchangia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu kama ifuatavyo:

1.Kutokunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kabla ya kula au baada ya kutoka chooni

2.Kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama

3.Kunywa maji yasiyo safi na salama

4.Kumuhudumia mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa huu bila kuzingatia kanuni za afya juu ya kuepuka kupata maambukizi.

5.Waandaji na upikaji wa chakula bila kuzingatia kanuni za afya


6.Usafirishaji olela kwa wagonjwa wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu ni vema kutoa taarifa iwepo kuna abiria mwenye dalili za ugonjwa huu ushauri namna ya kumsafirisha kwa namba ya simu -0767 300 234 ili ushauri uweze kutolewa

Idadi ya wagonjwa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam ni kama ifuatavyo:

1.Kinondoni ni wagonjwa 186

2.Ilala ni wagonjwa- 22

3.Temeke ni wagonjwa 22

Dk Seif alisema katika Manispaa ya Kinondoni wagonjwa wengi wanatoka, Makumbusho, Kimara, Tandale,Goba, Kibamba, Manzese, Magomeni, Mwanyamala, Kijitonyama,Kigogo na Mburahati’

Katika manispaa ya Ilala maeneo yaliyoathirika au wanapotokea wagonjwa wenye vimelea vya Ugonjwa wa Kipindupindu yakiwemo Buguruni, Tabata, Chanika, Shaurishamba na Ilala, Katika manispaa ya Temeke ni Mtoni kwa Azizi Ally, Keko, na Yombo Vituka’-
 
Top