Mimba Kutoka Mara Kwa Mara

Mimba kutoka mara kwa mara ni tatizo linalotokea kwa wajawazito ambapo mimba tatu au zaidi ambazo ni chini ya wiki 20 zimewahi kutoka. Hujulikana kama recurrent miscarriage au recurrent pregnancy loss. Karibu asilimia moja ya wanawake wenye uzazi hukumbwa na tatizo hili. Hatari ya tatizo hili kutokea huongezeka kadri umri wa mwanamke unavyoongezeka.
Sababu Za Mimba Kutoka Mara Kwa Mara

Kuna sababu mbalimbali za mimba kutoka mara kwa mara, hizi zinajumuisha:
  • Matatizo ya mji wa mimba ya kuzaliwa nayo (congenital malformation). Kizazi huwa hakina umbo au nafasi ya kutosha kuruhusu mtoto akue mpaka kuzaliwa.
  • Vivimbe vya mji wa uzazi (uterine fibroids)
  • Shingo ya Uzazi kulegea (cervical incompetence). Kadri mimba inavyokua, shingo ya uzazi hushindwa kuhimili na hivyo mimba hutoka.
  • Kushikana kwa kuta za mji wa mimba. Hujulikana kama Asherman’s Syndrome.
  • Kisukari
  • Ugonjwa wa vivimbe vya ovari (polycystic ovarian syndrome)
  • Kuvuta sigara
  • Upungufu wa homoni ya tezi shingo (hypothyirodism)
  • Ugonjwa wa thrombophilia.
  • Vichochezi kutokaa vizuri (hormonal imbalance)

Dalili Za Mimba Kutoka

Mara nyingi tatizo hili hutokea hasa mimba ikiwa bado changa, dalili zikijionesha wiki ya 10 au kuendelea kidogo. Mimba inayofuata kuharibika huwa katika wastani wa umri uleule wa mara ya kwanza au chini ya hapo kidiogo. Dalili kuu huwa;
  • Kutokwa na damu ukeni
  • Maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu na kiunoni
  • Kutoa uchafu au sehemu ya mimba iliyoharibika.
Wakati mwingine homa na kutapika vinaweza kuambatana na dalili hizo.

Uchunguzi Na Vipimo

Unapopata dalili zinazoashiria tatizo hili wahi uonane na daktari. Uchunguzi na vipimo hufanyika ilii kuweza kugundua chanzo cha tatizo hili. Ingawa mara nyingine inakuwa ni ngumu kujua chanzo halisi cha tatizo, hii isikukatishe tamaa.

Matibabu

Tatizo hili huleta msongo wa mawazo  na kukatisha tamaa kwa wenza wanaopitia hili. Ni muhimu kushirikia na kutiana moyo kwa karibu.
Karibu robo tatu ya wanawake wanaopata tatizo hili hupata ujauzito wa kawaida bila matibabu yoyote.
Baada ya vipimo na uchunguzi na cahnzo cha tatizo kujulikana, basi linaweza kutibiwa kisha tatizo likaisha. Matibabau yanaweza kuhusisha;
  • Dawa
  • Upasuaji
  • Kushona shingo ya uzazi kama imelegea (cervical cerclage)
 
Top