Lishe Bora Kwa Mtu Mwenye VVU/UKIMWI


 

Chakula gani kinafaa kwa mtu mwenye virusi vya ukimwi (VVU) au UKIMWI? Ni kati aya maswali ambayo huulizwa mara kwa mara na watu. Lishe bora ni muhimu sana kwa mtu mwenye VVU/UKIMWI, kwani mahitaji ya virutubisho  mwilini huongezeka na hivyo asipopata lishe bora ni rahisi kwa mtu mwenye VVU kuingia katika hali ya UKIMWI haraka, au mwenye UKIMWI kudhoofika zaidi.
Lishe Na VVU/UKIMWI
VVU/UKIMWI mara nyingi huathiri hali ya lishe kwenye mwili wa mtu, hii ni kwa kusababisha kukosa hamu ya kula, kutonyonywa chakula vizuri kutoka kwenye utumbo, kuharisha na kutapika. Hivi husababaisha upungufu wa virutubisho mwilini na hivyo mgonjwa kupata utapia mlo Utapia mlo husababisha mgonjwa kupungua uzito, kukonda, kinga ya mwili kudhoofika na hivyo kuptata magonjwa kwa urahisi.
Kwa hiyo ni muhimu sana kuhakikisha mtu mwenye VVU/UKIMWI anapata lishe nzuri ili kuhakikisha afya yake inaendelea vizuri.
Kama mtu mwingine ambaye hana virusi, mlo kamili ni muhimu kuhakikisha mgonjwa naapata virutubisho vyote muhimu. Hii hujumuisha vyakula vyenye Wanga, Protini, Mafuta, Vitamini na Madini. Mlo kamili huujenga mwili, kuimarisha kinga ya mwili na kusaidia kuzuia magonjwa.
Tafiti zinaonesha kuwa kuwa mtu mwenye VVU/UKIMWI anahitaji asilimia 10 -15 ya vyakula vya kutia nguvu (wanga –carbohydrates), na asilimia 50 – 100 ya vyakula vya protini zaidi ya mtu asiye na VVU/UKIMWI. Sambamba na vyakula hivyo, vitamini na madini nayo ni muhimu sana katika kuendeleza afya njema.
Njia za kuboresha lishe kwa mtu mwenye VVU/UKIMWI
  • Kula mlo mdogo mara kwa mara.
Hii ni kula kiasi kidogo cha chakula mara nyingi ndani ya siku moja. Badala ya kula milo 3 ndani ya siku moja, anaweza akala milo midogo midogo mara 5 au 6 ndani ya siku moja. Inasaidia zaidi pale mgonjwa anakosa hamu ya kula chakula au ana vidonda mdomoni.
  • Kula vyakula vya aina mbalimbali.
Kudumisha chakula bora ni muhimu katika afya ya mtu mwenye VVU/UKIMWI. Chakula bora kinapatikana kwa kula vyakula vya wanga, protini, mafuta,vitamini, madini na maji.
  • Kunywa maji masafi yaliyochemshwa
Kunywa maji safi yaliyochemshwa kila siku, angalau kiasi cha lita 2 (glasi 8) kwa siku. 
  • Tumia viungo  kuongeza ladha ya chakula
Viungo mbalimbali kama embe, limau, chachandu na kadhalika vinaweza kutumika kuongeza ladha ya chakula.
 
Top