Faida Za Matofe (Apple) Kiafya

Matofe ni tunda maarufu na linalopendwa sehemu mbalimbali duniani. Tunda hili limejaa virutubisho vya phytonutrients ambavyo ni muhimu kwa afya bora ya mwili. Tofe hujulikana kama apple kwa Kiingereza.

“An apple a day keeps the doctor away”  ni msemo maarufu kutokana na faida za tunda hili kwa afya ya mwili. Ingawa sio lazima ukila tofe kila siku hautaumwa, lakini utaboresha afya yako kwa kiasi kikubwa (ikiambatana na kufuata lishe bora).

Virutubisho Vilivyopo Kwenye Matofe

Matofe yana virutubisho vifuatavyo:
  • Wanga
  • Vitamini C
  • Kambakamba (dietary fibers)
  • Vitoasumu (antioxidants phyto-nutrientsflavonoids na polyphenolics
Matofe hayana fati wala lehemu.
Matofe yana kiasi kidogo cha wanga, na kiasi kikubwa cha kambakamba.

Faida za Matofe Kiafya


Husaidia kupunguza  na kuulinda mwili dhidi ya sumu za mwili (free radicals). Matofe yana vitoasumu vingi vya flavonoids napolyphenolics.
  • Hupunguza hatari ya kupata saratani
Kampaundi za flavonoids zilizopo  ndani ya matofe husaidia kuondoa sumu kwenye mwili ambazo huchangia utokeaji wa saratani.
  • Kuimarisha Kinga Ya Mwili
Matofe yana vitamini C kwa wingi ambayo husaidia kuimarisha kinga ya mwili ya vijidudu vya magonjwa.
  • Kulainisha Choo
Matofe yana kambakamba nyingi ambazo hulainisha choo, hivyo hupunguza tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu.
  • Kupunguza Lehemu Mwilini
Tofe lina kambakamba ambzo husaidia kunguza unyonyaji wa lehemu kutoka kwenye utumbo. Hii husaidia kupunguza lehemu mwilini.
  • Ufanyaji Kazi Wa Moyo
Matofe yana madini mbalimbali ikiwemo potasiamu kwa wingi ambayo husaidia ufanyaji kazi wa moyo vizuri.

Tahadhari

Baadhi ya watu wana allergy na matofe, kutokana na aina ya protini iliyo ndani ya matofe.
Ulaji wa mbegu za matofe unaweza kuhatarisha afya yako. Ukila mbegu nyingi sana, kama kikombe kimoja, inaweza kuleta sumu ya cyanide.
 
Top