Asante kwa wale ambao wameendelea kuuliza maswali mbalimbali kupitia namba zetu hizi zifuatazo 0769 400 800, 0784 300 300, 0716 300 200 lakini pia na kwenye ukurasa wetu wa  faceboo uitwao Mandai Herbalist Clinic -mhc.

Leo nimeona nijibu hili swali ambalo limekuwa likiulizwa na kinadada na kinamama wengi ambao wamehitaji kufahamu sababu zinazopelekea kupata maumivu ya matiti.


 
Nikianza kujibu swali hilo kwa faida ya wale waliouliza pamoja na wadau wa www.dkmandai.com, kwanza napenda ifahamike kuwa maumivu haya ya matiti huweza kutokea kwenye matiti yenyewe au pembeni yake (karibu na kwapa.) na kitaalamu tatizo hili hufahamika kama 'mastalgia'.

Mwanamke mwenye tatizo hili huweza kuhisi maumivu pale unapoyashika matiti, jambo ambalo hupelekea wanawake kupata hofu zaidi, huku wengine wakihisi kuwa ni dalili ya saratani.
 

Aidha, maumivu hayo yanaweza kuwa kwenye ziwa moja au maziwa yote, huku yakiambatana na kuvimba, uvimbe au mara chache kidonda. 

Kuna sababu mbalimbali ambazo husababisha maumivu  ya matiti kama hizi zifuatazo:
  • Kukoma kwa hedhi (menopause)
  • Hali ya mabadiliko ya vichocheo vya uzazi ambavyo hujitokeza kabla ya hedhi kuanza. hali hiyo huchangia matiti kujaa na kuuuma na kusababisha mumivu hayo.
  • Maambukizi ya matiti
  •  Matiti yanaweza kuwa na vivimbe visivyo saratani (cysts) ambavyo hujaa maji na kusababisha maumivu ya kujirudia rudia.
  • Kutanuka kwa mirija ya maziwa
  • Saratani ya matiti. Ni aghalabu sana kwa saratani ya matiti kusababisha maumivu ya matiti.
Hata hivyo, ni vyema ikafahamika kwamba mara nyingi maumivu ya matiti huisha yenyewe baada ya muda fulani. zifuatazo ni njia ambazo huweza kukupati ahueni ikiwa unatatizo hili:
  • Vaa sidiria isiyokubana
  • Punguza unywaji wa chai na kahawa
Ikiwa unaona hali inaendelea ni vyema kuonana na wataalam kwa ajili ya uchunguzi zaidia wa kiafya.
 
Top