LIJUE TATIZO LA KUOTA KINYAMA NJIA YA HAJA KUBWA (BAWASIRI)/HEMORRHOIDS
Leo ninaongelea kuhusu tatizo la bawasiri au hemorrhoids kwa lugha ya kiingereza.Tatizo hili huwapata watu wa umri tofauti tofauti na ni tatizo ambalo linagusa sehemu nyeti ya mwili wa binadamu, hivyo kusababisha watu wengi kuwa na aibu ya kwenda hospitali na kueleza juu ya tatizo hili kwa daktari. Bawasiri husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
A.KUNA AINA MBILI ZA BAWASIRI(HEMORRHOIDS)
1.Ya nje ya puru(external hemorrhoid)– Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na mara nyingi huambatana na maumivu na muwasho katika sehemu hiyo.Mara nyingi mishipa hiyo ya damu(vena)hupasuka na damu huganda na kusababisha hali iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS kitaalamu.
2.Ya ndani ya puru(internal hemorrhoid)-Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa na haiambatani na maumivu hivyo kuwafanya wengi kutotambua kuwa wana tatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika grades nne kama ifuatavyo kwa kadri ya ukubwa wa tatizo;
I.Bawasiri kutotoka katika mahali pake(iliyosimama)
II.Bawasiri inayotoka wakati wa haja kubwa kurudi yenyewe baada ya kumaliza kujisaidia
III.Bawasiri inayotoka wakati wa haja kubwa na hairudi yenyewe baada ya kujisaidia mpaka mwathirika airudishe mwenyewe.
IV.Bawasiri inayotoka wakati wa haja kubwa na ni vigumu mtu kuirudisha baada ya kumaliza kujisaidia.
B.NINI KINASABABISHA BAWASIRI ?
Miongoni mwa visababishi vya bawasir ni;
-Tatizo sugu la kuharisha
-Kupata haja kubwa(kinyesi)kigumu
-Ujauzito
-Uzito kupita kiasi(overweight/obesity)
-Umri mkubwa na mambo yanayoongeza shinikizo katika tumbo.
C.DALILI ZA BAWASIRI
-Kinyesi kuchanganyika na damu wakati wa kujisaidia (hematochezia)
-Maumivu wakati wa haja kubwa
-Kijiuvimbe katika eneo la tundu(mlango)wa kutolea haja kubwa.
-Ngozi katika eneo la tundu la haja kubwa kuwasha.
-Bawasiri kutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa.
D.ATHARI ZA BAWASIRI
-Maumivu wakati wa haja kubwa,
-Kukupunguzia morali ya kufanya kazi kutokana na maumivu hasa watu wanaokaa muda mrefu maofisini.
-Kuathirika kisaikolojia
E.JINSI YA KUZUIA BAWASIRI
-Kula mboga za majani na matunda na nafaka zisizokobolewa kwa wingi
-Kunywa maji mengi angalau lita 3 kwa siku.
-Punguza kukaa kwa muda mrefu sana ukiwa chooni(unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa)
MATIBABU
-Mara nyingi dawa iliyo kubwa ni kukatwa kinyama na uendelee kula vyakula vinavyolainisha choo pamoja na vilainisha-choo(laxatives) ingawa mara nyingi ugonjwa hurudi tena, na kuhitaji upasuaji ili kuondoa vinyama hivi.