Habari rafiki, natumaini mnaendelea vizuri na kuendelea kuelimika katika blog hii, napenda kumshukuru Mungu kwa kunijaalia Afya kuweza kuandika makala hii inayohusu uvimbe katika mayai ya mwanamke hivyo ungana nami rafiki kupata elimu hii.

OVARIAN CYST NI NINI???
~Ni uvimbe unaotokea katika mayai ya mwanamke(ovarian)
~uvimbe huo hutokana na mkusanyiko wa maji maji yanayozungukwa na kutu nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke
~mara nyingi tatizo hili hutokea kwa wanawake wa rika tofauti na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofika umri wa kushika ujauzito, pia uvimbe huo huweza kuwa wa ukubwa wa cm3_cm30 na unaweza kujaza tumbo lote na kufanya uonekane mjamzito

AINA KUU ZA UVIMBE KATIKA MAYAI YA MWANAMKE
(@)HEMORRHAGIC CYST ~hii ni Aina ya uvimbe ambayo hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa Aina yoyote ule ambao umeshajitengeza tayari
~mara nyingi uvimbe huu huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja mmoja (kushoto/kulia)
(@)FOLLICULAR CYST ~hii ni Aina ya uvimbe unaotokea wakati ovulation isipotokea au baada ya corpus luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi
~uvimbe huu huwa na wastani wa nchi 2:3 kwa upana, na huwa hauna dalili yoyote na mara nyingi huwa unapotea wenyewe
(@)CORPUS LUTEUM CYST ~hii ni Aina ya uvimbe ambao hutokana na kutopachikwa kwa yai lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi
~uvimbe huu husinyaa na kupotea wenyewe ingawa wakati mwingine huweza kujaa maji na kusababisha tumbo kuvimba upande mmoja
(@)DERMOID CYST ~huu ni uvimbe unaojulikana kama MATURE CYST TERATOMA, uvimbe huu huwaathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika ujauzito,
~uvimbe huu huweza kuwa na ukubwa wa nch 6 kwa upana na ndani Yake huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mifupa, mafuta na cartilage pia uvimbe huu huweza kuwa mkubwa zaidi na kujizungusha hivyo huathiri mzunguko wa damu na hivyo kusababisha maumivu makali ya tumbo
(@)POLYCYSITIC APPEARING CYST ~huu ni uvimbe mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijiuvimbe vingi vidogovidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye Afya njema na hasa wale wenye tatizo la homoni (hormone imbalance)
(@)CYSTEDONOMA ~hii ni Aina ya uvimbe unaotokea kwenye tishu za ovary na hujazwa na maji maji Aina ya kamasi, pia uvimbe huu una ukubwa wa kuanzia nchi 12au zaidi kwa upana
(@)ENDOMETRIOSIS/ENDOMETRIAL CYST ~hii ni uvimbe unaosababishwa na uwepo wa Aina mojawapo ya kuta za mfuko wa kizazi unaojulikana kama ENDOMETRIUM kwenye mayai ya mwanamke
~uvimbe huu huathiri wanawake walio katika umri wa kushika ujauzito na huambatana na maumivu makali ya nyonga (CHRONIC PELVIC PAIN) wakati wa hedhi
~uvimbe huu una rangi nyekundu ya kahawia (reddish brown)na una ukubwa wa 0.75_8 inches

 VIHATARISHI VYA TATIZO HILI
~👉kuwa na mzunguko wa hedhi usioeleweka (IRREGULAR MENSTRUATION CYCLE)
👉kuwa na mafuta mengi tumboni
👉kukosekana kwa uwiano wa vichocheo mwilini (hormone imbalance)
👉kuvunja ungo mapema (katika umri wa miaka 11_kushuka chini)
👉kutumia dawa za matibabu ya saratani ya matiti (tamoxifen)
👉ugumba

DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO HILI
👉kupata maumivu makali ambayo huchoma katika nyonga, uke, tumbo, mapajani, mgongoni NK
👉kuhisi tumbo kuwa zito limejaa au kuvimba
👉kupata maumivu katika matiti
👉kutopata hedhi katika mpangilio
👉kuvimbiwa mara kwa mara
👉kuongezeka uzito haraka
👉kupata maumivu katika mbavu
👉nywele kukua haraka kila wakati
👉kupata maumivu makali wakati wa hedhi
👉kuhisi kichefuchefu
👉kupata maumivu ya nyonga kila unapofanya mapenzi, mazoezi, Kazi ngumu
👉kuhisi uchovu kila wakati
👉kutokwa na matone ya damu
👉kutoshika mimba
👉mabadiliko katika upatikanaji wa haja
@haja ndogo kutoka Bila kujielewa
(b) haja kubwa kuwa ngumu

VIPIMO NA MATIBABU
~Kuna vipimo vingi vya kuona tatizo hili kama vile
(@)ENDOVAGINAL ULTRASOUND, COMPLETE BLOOD COUNT, SERUM CA_125 ASSAY, hivyo ndio vipimo vya kuona tatizo hili kama lipo pia matibabu ya tatizo hili yamegawanyika katika sehemu kuu mbili
(A) MATIBABU YA DAWA
~Tiba hii huhusisha matumizi ya dawa za uzazi wa mpango kwa Muda wa miez 4_6,
~matumizi ya dawa Hizi kwa Muda mrefu huzuia kutokea tena kwa uvimbe katika mayai ya mwanamke kwasababu dawa Hizi hufanya Kazi kwa kuzuia mayai kutoa mayai ya uzazi (ovums) Lakini dawa hizi hazipunguzi uvimbe kwani uvimbe hupotea wenyewe baada ya Muda
(B) MATIBABU YA UPASUAJI
~tiba hii imegawanyika katika madaraja mawili yafuatayo
(1)EXPLORATORY LAPARATOMY
~Hapa mgonjwa hupasuliwa tumboni na daktari huweza kuondoa uvimbe
~upasuaj huu hufanyika kwa wanawake wenye uvimbe mkubwa ambao haupotei yani uvimbe wa 5cm_10 cm
(2)LAPARASCOPIC SURGERY
~huu ni upasuaji ambao daktari hupasua sehem ndogo na kutumbukiza mpira maalumu ambao una kamera kwa mbele na huondoa uvimbe katika mayai ya mwanamke, pia upasuaji huu hupendwa na wanawake wengi kwasababu hauachi kovu lolote,
~tiba hii ni kwa uvimbe mdogo hata hivyo Kuna uwezekano wa tatizo kujirudia
NOTED :ndugu rafiki hakikisha unaenda kupima Afya yako kila mwezi ili kujua maendeleo ya Afya yako kwasababu madhara ya tatizo hili ni Kuja kuwa mgumba pia huweza kusababisha saratani
 
Top