Ulimwengu hauna mwanga sehemu zote kwa wakati mmoja, ni kama hivyo tu, vitu hutokea, na tunashikwa, na kusahau kuhusu kila kitu muhimu.

Mara nyingine tunakosa amani , tunakuwa hatuna furaha, tunatazama na kuona watu wengine wana furaha , na tunabaki kushangaa tuna matatizo gani sisi. Kwa nini tuna matatizo na hatuna furaha?

Kwa hio , kwanza kitu cha kwanza, unahitaji kuelewa kwamba hata watu wenye furaha ya kweli hawawezi kuwa na furaha siku zote, muda wote. Wanaweza, ingawa wana vitu vya ndani vinavyowaunganisha na hio sababu , panapotokea vitu vibaya na wakati huo walikuwepo kwenye furaha. wanakuwa na mwitikio wao wa kukubaliana na yaliotokea ndio wana nguvu hio. Kwa ujumla, wanafuraha haijalishi ni kitu gani kimetokea.

Inasikitisha, si kila mtu ana huo muunganiko wa hisia za ndani zinazojizalisha kuendeleza furaha ya mtu. Kusema kweli, watu wengi hawana. Ingawa, kwa kutumia nguvu kidogo za kujitafutia furaha. Madhara yake huonekana kwa urahisi. Ukweli , unaweza kufanya hivyo haijalishi unajisikiaje kwa wakati huo, tumia hizi mbinu tatu kwa ajili ya kuwa na furaha.

1.Reframe it. 
Kinapotokea kitu kibaya, badaya ya kuangalia negative, unaweza kutazama mtazamo mpya ,kwa njia ya uzuri ,’’ positive way’’angalau kwa kitu cha tofauti , kama umefukuzwa kazi kwa mfano, badala ya kuona aibu na wasiwasi na woga wa maisha yako mbele, usione hio aibu , ona ni jambo la kawaida ambalo lingemtokea mtu yeyote. Lakini watu wenye furaha huona kufukuzwa kazi kuwa ni nafasi ya kupata kitu kingine kipya na kizuri zaidi ya hicho .

Inaweza kuwa ni nafasi ya kurudi tena shule, ili kuanza ujuzi mpya, au kutafuta kazi mpya kwenye kampuni nzuri zaidi au kuepukana na bosi mwenye roho mbaya kwako, au kukaa nyumbani kutunza watoto au vyovyote, kumbuka, chochote kinachotokea katika maisha, lazima kuna njia nyingine mbadala na ni nzuri kwako. Watu wengi walishagundua hilo , kwamba ukifungwa mlango huu, utafunguliwa mwingine. Inawasaidia kuelewa ukweli wa thamani.

2.Connect 
Watu wenye furaha hubaki kwenye mawasiliano na wale wawapendao, hasa wenza wao, marafiki wa karibu, na familia walio nayo. Hupenda kurudi kwenye hisia zao za kirafiki wakati vitu vinapokuwa vizuri kwao na hata maisha yanapokuwa magumu sana. Huelewa nini maana ya kuwa na furaha, wanaelewa kuwa furaha hushirikishwa na furaha wakati huzuni hushirikishwa na huzuni nusu. Kwa hio unapojisikia kushuka moyo nenda kwa watu wanaojali na uwaambie nini kinaendelea wakati huo.

Kitu rahisi cha kufanya hivi, hata kama utaona haibadilishi hali halisi unayosumbuka nayo , itasaidia kuboresha hali yako kadri unavyokuwa nao. Inakubidi ukomae katika ustawi wa wengine kwa muda kidogo, hasa wale wenye hali nzuri kuliko wewe. Kwa kujitolea au kutoa muda wako, utaalamu, na upendo ni kwa njia zingine.

3.Uwe na shukrani. 
Katika mafunzo mengi , na kupitia wachunguzi wengi , na hata kila rika , dini , siasa , na hata wataalamu wa jinsia , kulenga katika kazi yenye furaha . niligundua tofauti moja ya msingi kati ya wale wenye furaha na wale wasio na furaha, wanafurahia kwa kile walichonacho na pia wanashukuru kwa hilo. Na pia haijalishi walichonacho, ili mradi wanashukuru kwa kwa hayo.

Wanakuwa wanaangalia zaidi nguvu kuliko udhaifu wao. Na kwa kawaida wana reframe matatizo mara kwa mara huunganika na wengine. Kwa sababu hio wana matumaini makubwa , kuliko msisitizo. Ukijikuta unahangaika na shukurani , chukua kalamu na karatasi andika vitu 10 vya shukrani. Usiogope kuonyesha shukrani ya kweli ambayo ipo kichwani mwako. Chakula ndani mwako, hewa safi, maji safi na zidi ya hivyo. Unaweza kuongezea , nguvu ulizonazo, kazi ulionayo, familia, marafiki, hata uwezo ulionao, hata tabasamu ulilonalo, ukifanya hivyo, matokeo yake yatakushangaza sana

Tafuta furaha kila wakati.
 
Top