Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una Vitamin C nyingi kuliko hata machungwa na ina kiwango kingi cha madini ya kashiamu (Calcium) kuliko hata maziwa ya ng’ombe.
Aidha, unga wa ubuyu ni chanzo kikubwa cha madini mengine aina ya chuma (iron), Potasiamu (Pottasium) na manganizi (magnesium). Inaelezwa kuwa kiwangao cha Potasiamu kilichomo kwenye unga wa ubuyu ni mara sita zaidi ya kile kinachopatikana kwenye ndizi. Ubuyu ni muhimu sana kwa watu wenye matatizo ya figo.
Vile vile unga wa ubuyu una uwezo mkubwa wa kuongeza kinga ya mwili  (antioxidant) kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vya kuongeza kinga mwilini dhidi ya magonjwa nyemelezi. Kiwango chake kinazidi hata kile kinachotolewa na matunda mengine kama vile Krenberi, bluberi na blakberi. Ili upate faida za unga wa ubuyu zinazoelezwa hapa, lazima ule ubuyu halisi usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha.
 

MAFUTA YA UBUYU
Mafuta ya ubuyu, ambayo hutengenezwa kutokana na mbegu zake, ni mazuri kwa kulainisha ngozi na kukarabati au kuponya ngozi iliyoathiriwa na magonjwa ya ngozi mbalimbali, ikiwemo fangasi, vipele na chunusi.
Mafuta ya ubuyu yana uwezo wa kuifanya ngozi kuwa nyororo na laini kutokana na kuwa na kiasi kingi cha mafuta aina ya Omega 3 na Omega 6 na ina kiasi kingi cha Vitamin A, D na E ambazo zote ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa ngozi ya binadamu.
Mafuta ya ubuyu yanaelezwa kuwa na virutubisho vinavyoweza kuondoa mikunjo ya ngozi, mabaka, michirizi na hata makunyazi na kuicha ngozi kuwa mpya. Hutoa kinga dhidi ya uharibifu wowote wa ngozi unaoweza kujitokeza baadaye.

Kwa ufupi mafuta ya ubuyu yana Virutubisho vifuatavyo:
  • -Vitamin:  (Thiamin) vitamin B1, Riboflavin) B2, (Niacin) B3, kiasi kikubwa cha (Ascorbic Acid) Vitamin C, Vitamin A, Vitamin D, Antioxidant na Vitamin E (Tocopherol)
  • -Madini kama vile: – kiasi kikubwa cha Calcium, Manganese, Iron, Potassium, Zinc, Phosphorus, na Amino acids 

FAIDA ZAKE:- 

  • Yanakuongezea hamu ya kula na kukumbuka vizuri kwa ufasaha kutokana na kiwango kikubwa cha vitamin B complex zilizomo. kwa hiyo ni mazuri kwa wakubwa na watoto
  • Yanasaidia kunyonywa kwa vitamin B12 kwenye tumbo kutokana na kiwango kikubwa cha ascorbic acid, ambayo ni muhimu kwenye kutengeneza chembe hai nyekundu na kukuepusha na Anemia.
  • Yanasaidia kusafisha mfumo wa chakula na kufunga tumbo la kuhara zaidi kwenye unga  wa ubuyu kutokana na uwepo wa “roughage” nyingi.
  • Yanasaidia mtu  kuona vizuri kutokana na uwepo wa Vitamin A ndani yake.
  • Mazuri kwa Walemavu wa Ngozi kama (Albino) Kutokana na uwepo wa vitamin A, Vitamin D na Vitamin E (Tocopherol).
  • Ni mazuri pia kwa watoto wadogo na  wajawazito kwa ajili  ya kuimarisha mifupa hasa  kuanzia miezi sita hadi tisa ya ujauzito (third tremester), hiki ni kipindi ambacho mtoto anatengeneza na kuimarisha mifupa yake akiwa tumboni kwa mama yake, hii ni kwasababu ya kiwango kikubwa cha Calcium na vitamin D, na vitamin A.
  • Mafuta haya ni mazuri kwa kupunguza vitambi kutokana na uwepo wa Omega 3.
  • Hurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
  • Hurekebisha shinikizo la damu (pressure).
  • Yanasaidia kuongeza kinga ya mwili yaani CD+4, zaidi kwa wagonjwa wa ukimwi, kansa, au watu waliougua kwa muda mrefu na wanawake wanapokuwa katika hedhi wanaweza kutumia.
MATUMIZI YA MAFUTA YA UBUYU:-Tumia vijiko viwili vya mafuta kwenye kijiko cha chai, kisha changanya kwenye glasi ya maji, juisi, maziwa,( yanaweza kuwa mtindi au freshi), soda, asali n.k, au unaweza kunywa bila kuchanganya na kitu kingine. Tumia hivyo  mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa mafanikio mema na matokeo mazuri. 
Mafuta ya ubuyu unaweza kuyatumia kwa kupaka usoni au mwili mzima moja kwa moja. Unaweza kuyatumia mafuta haya kwa kupaka sehemu tu iliyoathiriwa kama dawa. Unaweza pia kuchanganya na mafuta au losheni unayotumia.
Ili kupata matokeo unayotarajia, hakikisha unatumia mafuta halisi ya ubuyu ambayo hayajachanganywa na kitu kingine wakati wa kutengeneza.
 

UPATIKANAJI WAKE
Bidhaa za ubuyu zimeanza kujipatia umaarufu nchini Tanzania na hivi sasa kuna makampuni na wajasiriamali binafsi wanaojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na ubuyu, hivyo upatikanaji wake ni rahisi iwapo utaulizia maeneo unayoishi.
Bidhaa zingine zinazoweza kutengenezwa kutokana na mti huu ni pamoja na majani yake ambayo hutumika kama dawa, mizizi na magamba yake pia. Kwa ujumla mti wote wa ubuyu una faida na hakuna kitu kinachotupwa kwenye mti huu ambao ni miongoni mwa miti yenye matunda bora yaliyopewa jina la ‘superfruit’.
 
Top