pumu 2
Ugonjwa wa pumu hutokana na uvimbe au kubana kwa njia ya hewa kunakotokana na kusinyaa kwa misuli katika kuta za njia za hewa. Matokeo yake ni kupumua kwa shida na kukosa hewa ya kutosha. Ni ugonjwa wa kudumu usio na tiba ya moja kwa moja, ila kuna dawa na matibabu mengi yanayosaidia kutanua njia ya hewa na kuondoa tatizo hili pamoja na kuboresha maisha ya mgonjwa.
Huwakumba watu wa jinsia zote na mara nyingi huanzia utotoni. Baadhi ya wagonjwa wa pumu huweza kupona kabisa wakifikisha miaka 12 au utu uzima.
VITU VINAVYOSABABISHA AU KUONGEZA PUMU
pumu 1 





















Mfumo wa upumuaji wa mwanadamu. Ndiyo sehemu kuu inayohusika na ugonjwa huu. Pia ndiyo sehemu kuu inayohusika na hewa tunayovuta ndani na hewa tunayotoa nje, uvutaji wa sigara na madhara yake. Sigara pia inaweza kuchochea tatizo hili



Kama tulivyoona hapo juu pumu hutokana na uvimbe au kubana kwa njia ya hewa kunakokotokana na kusinyaa kwa misuli. Uvimbe au kubana kwa njia ya hewa kunaratibiwa na kinga ya mwili yenyewe, na huweza kuchochewa na vitu kama vile:
  1. Vumbi
  2. Harufu/Chembechembe za rangi za nyumba, magari nk
  3. Manukato (Pafyumu na vipodozi vingine vyenye harufu kali)
  4. Poleni za maua
  5. Baadhi ya dawa
  6. Hali ya hewa ya mawingu/unyevuunyevu mwingi kwenye hewa
  7. Baadhi ya vyakula
  8. Nywele na manyoya ya wanyama (Mfano paka)
Kimsingi vingi kati ya hivyo ni kemikali au vitu vinavyoweza kuchochea mwili kisha mwili kuviona ni vitu vigeni na kuanza kujilinda au kuvishambulia ndani kwa ndani.
Na ni kweli hata kwenye mazingira ya kawaida. Mtu mwenye pumu anaweza akawa sawa kabisa, lakini akipita sehemu yenye vumbi au poleni za maua au hali ya hewa ikibadilika na kuwa ya mawingu tu basi pumu yake huanza na anakuwa mgonjwa. Pia kadiri anavyozidi kuendelea kuwa katika mazingira hayo ndivyo ambavyo pumu inakuwa inaongezeka.
JINSI YA KUJIKINGA DHIDI YA PUMU
Kwa mtu ambaye ana ugonjwa huu njia nzuri zaidi ya kujikinga ili pumu isimuanzie na kumsumbua ni kujiepusha na vitu vyote vinavyomsababishia au vinavyoweza kumsababishia au kumuongezea tatizo la pumu. Ajiepushe na vitu kama vile:
  1. Vumbi
  2. Harufu/Chembechembe za rangi za nyumba, magari nk
  3. Manukato (Pafyumu na vipodozi vingine vyenye harufu kali)
  4. Poleni za maua
  5. Baadhi ya dawa
  6. Hali ya hewa ya mawingu/unyevuunyevu mwingi kwenye hewa
  7. Baadhi ya vyakula
  8. Nywele na manyoya ya wanyama (Mfano paka)
MATIBABU YA PUMU
pumu
Matibabu ya pumu yanategemea sana kiasi ambacho mtu anaumwa (ukali wa pumu yenyewe). Kuna kubanwa kidogo, kubanwa kwa kati na kubanwa sana.
Dawa zipo nyingi sana na zipo katika mtindo mbalimbali kiasi kwamba zinaweza kumsaidia mtu mwenye pumu ya aina yoyote. Kuna za vidonge, za maji, za sindano, za kupulizia na za kuvuta.
Mifano ya dawa zake ni Salbutamolbudesonidebeclomethasoneaminophylline nk
Tahadhari : Dawa zote hapo juu zimetajwa kwa ajili ya mifano tu, na sio vinginevyo. Usinunue wala kutumia dawa yoyote bila kushauriwa na daktari. 
Muda mwingine inahitajika mtu apate dawa zaidi ya moja au apumzishwe kwa muda huku akiendelea na matibabu hospitali.
Kwa kifupi, kuna dawa na matibabu ya aina mbalimbali ya pumu na ni miongoni mwa magonjwa yanayotibika kabisa endapo utapata ushauri, dawa na matibabu mazuri kutoka kwa wataalam.
Usiteseke na pumu. Pata ushauri mzuri na matibabu mazuri. Tumia dawa mzuri kadiri unavyoweza na utaishi kwa amani siku zote.
Tunakutakia afya njema!
 
Top