Kama
ulikuwa hujui ngoja nikufahamishe, Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa
huko nchini Uingereza umebaini kuwa kulala chumba chenye mwanga
uliopitiliza kumehusishwa na mtu kuongeza unene wa kupindukia.
Timu ya watafiti kutoka Taasisi ya saratani ya jijini London imebaini
kuwa wanawake wana nafasi kubwa ya kuongezeka unene kwa kulala vyumba
vyenye mwanga mkubwa.
Hata hivyo utafiti huo unaonya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuwa
sasa watu waanze kununua mapazia mazito au ulazima wa kuzima taa wakati
wa kulala.
Sasa jiulize kibongobongo hii imekaaje kutokana na mazingira ya nyumba zetu?