WAPO ambao wakati wanapofanya mapenzi badala ya kupata furaha, wao wanasikia maumivu, wanaume ni mara chache sana kulinganisha na wanawake. Mwanamke ndiye husumbuliwa zaidi na tatizo hili. Mwanamke anaweza kukosa kuhisi furaha na matokeo yake kuumia wakati tendo linapoanza pale mwanzoni, ukeni au kwa ndani zaidi. Maumivu haya pia yanaweza kugawanyika katika makundi mawili. Kwanza ni maumivu wakati wa tendo la ndoa ambapo ndiyo hayo tuliyoyaona hapo juu na maumivu baada ya tendo. KUPATA MAUMIVU WAKATI WA TENDO Maumivu haya hutokea pale mwanamke anapoanza kukutana kimwili na mwanaume na mara nyingi hutokana na uke kuwa mkavu.Hii inaweza kusababishwa na maandalizi hafifu ya kabla ya tendo lenyewe na matatizo katika mfumo wa homoni au kupoteza msisimko wa hamu ya tendo hilo. 

 
Top