Watafiti
wanaoishi katika kipindi hiki tulicho nacho wamejitahidi sana kuithibitisha
ile kweli iliyothibitishwa kwanza na Biblia kwa kutoa maelezo haya:
Wanadamu ni viumbe kamili. Mara nyingi kile tunachokigawa katika sehemu
za kimwili, kiakili, na kiroho ni sehemu za mtu zilizo na uwiano unaoingiliana,
wala hazitenganishiki. Kwa maneno mengine, kinachoidhuru akili, kinaudhuru
mwili.Hali yetu ya kiroho ina shinikizo lake juu ya hali yetu ya kimwili,
na kinyume chake. Sisi ni watu kamili.
Kwa
mfano watafiti wa kisayansi katika uchunguzi wao uliodhibitiwa wamegundua
kwamba kicheko kile kitokanacho na furaha na shangwe huleta mabadiliko
yanayoweza kupimwa katika mfumo wa kinga mwilini mwa mtu. Unaweza kabisa
kuusaidia mwili wako kupigana na ugonjwa kwa vizuri zaidi ukiwa na furaha!
Uchunguzi huo huonyesha jinsi akili na mwili vinavyofanya kazi yao kwa
pamoja kwa ushirikiano wa karibu sana.
Katika
maelfu ya miaka iliyopita Neno la Mungu lilidokeza kuwapo kwa uhusiano
huo wenye nguvu kati ya akili na mwili ambao ni hivi karibuni tu umekubaliwa
na kuingizwa katika nadharia ya kiganga:
"Moyo uliochangamka ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka huikausha mifupa" - (Mithali 17:22)
"Moyo uliochangamka ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka huikausha mifupa" - (Mithali 17:22)
Kulingana
na mtume Yohana, Je, Ni kwa karibu jinsi gani uhusiano huo uliopo kati
ya akili na mwili unaathiri usitawi wetu wa kiroho?
"Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni" - (3 Yohana 1:2).
"Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni" - (3 Yohana 1:2).
Muumbaji
wetu anataka sisi tupate " kufurahia kuwa na afya njema "
Neno la Mungu linaweza kutumika kama chemchem yetu ya afya, pamoja na
kuwa chemchem yetu ya uzima wa milele.
Kwa
kuwa usitawi wetu kimwili na kiakili na kiroho unakwenda bega kwa bega,
Paulo anatoa kwetu ombi hili:
"Mlapo mnywapo au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" - (1 Wakorintho 10:31).
"Mlapo mnywapo au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" - (1 Wakorintho 10:31).
Injili
inajumuisha mambo yote mawili, uponyaji wa mwili na uponyaji wa roho.
Mtindo wa maisha uletao afya unaweza kutusaidia sisi kuwa Wakristo wenye
uchangamfu mwingi.
Hapa
zipo kanuni nane za kufuata endapo wewe kweli unataka kuishi maisha
yenye afya na yenye manufaa mengi zaidi.
1.
Hewa Safi
Hewa
safi ya nje, ni ya lazima kwa afya nzuri. Wakati wa mchana na wakati
wa kulala usiku, kuingiza na kuitoa hewa kwa njia inayofaa katika nyumba
zetu na mahali petu pa kazi hutuhakikishia kwamba damu yetu daima itagawa
oksijeni ya kutosha kila sehemu ya mwili wetu. Kuvuta pumzi nyingi wakati
wa matembezi ya asubuhi ni njia kuu ya kuupatia mwili wako oksijeni.
Aina
ya hewa tuivutayo ni dhahiri kwamba ni ya maana. Jihadhari usikae mahali
penye moshi au mvuke mwingi, penye hewa mbaya au hewa inayochukua vijimea
vidogo sana (bacteria) kutoka mahali fulani palipojificha.
Kuvuta
tumbako huichafua sana hewa na ni mojawapo ya wauaji wakuu wa siku hizi.
Utafiti wa sayansi umethibitisha kuwapo kwa uhusiano unaoleta madhara
kati ya tumbako na kansa ya mapafu, ugonjwa wa kuvimba mapafu na kupumua
kwa shida ( emphysema) na ugonjwa wa moyo. Mazoea ya mwili kuhusiana
na hiyo sumu ya nikotini katika sigareti hufanya uvutaji huo wa sigara
(tumbako) uwe mmojawapo wa mazoea magumu kabisa kuachana hayo. Kuvuta
tumbako kutaweza kuwaua watu milioni 12 kwa mwaka kufukia mwaka wa 2020
endapo mwendo huu wa sasa utaendelea
2.
Mwanga Wa Jua
"Faida
za mwanga wa jua ni nyingi:
1.
Dakika kumi na tano hadi 30 za kupata mwanga wa jua kila siku katika
ile sehemu ya mwanzo ya asubuhi au baadaye mchana alasiri husaidia mwili
kukusanya pamoja au kutengeneza Vitamini D yake wenyewe, kirutubisho
muhimu/homoni ndani ya ngozi. Vitamini D huisaidia damu kutengeneza
kalisi (calcium) na fosforasi, inayoijenga na kuitengeneza mifupa.
2.
Mwanga wa jua unafanya kazi yake kama dawa ya kuvika viini vya maradhi
na kuua vijimea vidogo sana (bacteria)
3.
Jua linatoa nguvu ambayo kwa hiyo mimea inaweza kuigeuza kaboni dioksidi
na maji kuwa kabohidreti [chakula cha wanga]… Bila ya njia hiyo
wanyama na wanadamu wangekufa kwa njaa
4.
Jua pia linamsaidia mwanadamu kujirekebisha na kukabiliana na kazi ya
usiku na kupunguza unyong'onyevu (depression) unaotokana na siku za
giza wakati majira ya baridi kali yanapotokea.
Neno
la tahadhari: Mwanga wa jua unaweza pia kuleta madhara kukaa kwa muda
mrefu kwenye mwanga wa jua kunaweza kuiunguza ngozi, kunaweza kuongeza
hatari ya kupatwa na kansa ya ngozi kunaweza kuharakisha kuzeeka, kunaweza
kuyaharibu macho, na kusababisha mtoto wa jicho (cataracts). "
[Madondoo yote katika Mwongozo huu yamenukuliwa kutoka katika Look up
and Live: A Guide to Health, Lesoni ya Watu Wazima, Robo ya kwanza ya
mwaka wa 1993, (Nampa, Idaho: Pacific Prexss Publishing Association).
Mambo mengi katika Mwongozo huu ambayo hayajawekwa katika Alama za kunukuu
yamefundishwa kutoka katika lesoni hiyo hiyo]
3.
Kupumzika
Mwili
huu ni lazima upumzike ili upate kujitengeneza upya wenyewe. Yatupasa
kuwa na muda wa burudani na wa kupumzika ili kupunguza msongo utokanao
na kazi pamoja na majukumu ya kifamilia. Bila kuwa na muda wa kutosha
kupumzika mara nyingi watu wanakuwa na wasiwasi, mfadhaiko na hasira
kali. Msongo huo wa moyo unaweza kuleta ugonjwa ambao utatulazimisha
kuchukua pumziko letu ambalo miili yetu ilikuwa inataka kwa muda wote.
Hakuna kitu cha badala cha kuweka mahali pa usingizi mzuri wa usiku.
Kuzichaji
upya betri zetu za kiroho kwa kuweka utaratibu wa kila siku ni muhimu
pia kwa afya yetu ya kimwili. Muda wa kila siku anaotumia Mkristo katika
kutafakari, kusoma Biblia, na maombi utaweza kuuponya mwili pamoja na
roho. Tunakuhitaji pia kupata pumziko ili kuuvunja mzunguko wa kazi,
yaani, kuwa na siku ya kupumzika kila juma, na likizo ya mwaka au nusu
mwaka.
4.
Mazoezi Ya Mwili
Mazoezi
ya mwili ni ya muhimu sana kwa afya yetu:
1. Mazoezi ya mwili husaidia kulirekebisha shinikizo la damu.
2. Mazoezi ya mwili huiruhusu damu nyingi zaidi kuzifikia sehemu zote za mwili na kuifanya mikono na miguu ipate joto.
3. Mazoezi ya mwili yanaondoa mambo yote mawili. Yaani mkazo wa mwili na mfadhaiko wa moyo, na kukusiadia wewe kujisikia vizuri zaidi katika maisha yako. Mazoezi ya mwili kwa kawaida ni tiba bora kabisa ya wasiwasi na msongo (stress).
4. Mazoezi ya mwili hutupatia nguvu ya umeme kwa ajili ya ubongo wetu pamoja na seli za neva. Yanaongeza afya kwa kuuamsha mfumo wa kinga mwilini (immune system). Mwili unapowekwa katika hali ya afya kwa kufanya mazoezi yanayofaa. Ubongo unakuwa na uwezo wa kufikiri kwa ubunifu na ufanisi zaidi.
5. Yanaweza kukusaidia kuiweka vizuri rangi ya uso wako na kukuweka katika hali nzuri kabisa kimwili.
6. Mazoezi ya mwili hukufanya uwe na nguvu nyingi zaidi, hivyo kuchelewesha kupatwa na uchovu kimwili na kimawazo
7. Yanausaidia ubongo wako kutengeneza dawa inayokupa wewe hali ya kujisikia vizuri na kukuongezea uwezo wa kustahimili maumivu.

Endapo
wewe ulikuwa hufanyi mazoezi, basi anza taratibu (polepole) na kuongeza
nguvu yake hatua kwa hatua upatapo uwezo wa kustahimili. Laweza kuwa
ni jambo la busara kumwona mganga wako kabla ya kuanza mazoezi hayo.
Lengo lako na liwe kujishughulisha na kila aina ya mazoezi hayo ya mwili
ambayo yanaweza kulinganishwa na kutembea maili moja kwa dakika kumi
na tano mara nne au zaidi kw ajuma.
5.
Maji
Kwa
vile maji ni ya lazima kwa kila seli mwilini, basi, ingetupasa kunywa
maji mengi.
1. Kwa uzito, mwili wetu karibu asilimia sabini ni maji…
2. Mwili wetu unahitaji takribani visaga (quarts) viwili na nusu vya maji kila siku ili uweze kufanya kazi zake zote. Baadhi ya kazi hizo ni pamoja na mzunguko wa damu mwilini, kuondoa uchafu mwilini, kusafirisha virutubisho vya chakula mwilini, na kukiyeyusha chakula mwilini
3. Mtu wa kawaida anazo seli za ubongo kati ya billioni 15 na 40 hivi. Kila moja ya hizo ina maji asilimia 70 hadi 85. Maji ya kutosha kuweza kuzigawa seli hizo hukufanya uwe na akili iliyochangamka, halafu husaidia kuzuia mfadhaiko (depression) na hasira kali.
4. Si maji yale tu unayokunywa ambayo ni ya muhimu. Kuoga maji ya baridi kidogo au vuguvuvugu kila siku au kwa kutumia bafu ya manyunyu (shower) huboresha mzunguko wa damu mwilini, hivyo kuupa mwili na ubongo wako nguvu. Bafu ya manyunyu au kuoga kwa njia ya kawaida huweza pia kutuliza mishipa ya fahamu iliyochachamaa, ambayo inaweza kuleta ugonjwa kwa kudhoofisha mfumo wa kinga mwilini. Kuoga pia kunaondoa uchafu kutoka juu ya ngozi, pia kunaweza kupunguzahoma.

6.
Lishe Ifaayo
Wakati
ule wa uumbaji Mungu alimwagiza Adamu na Hawa kula chakula cha kokwa,
nafaka na matunda (Mwanzo 1:29). Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi,
ziliongezwa mboga za majani katika lishe yao
(Mwanzo 3:18). Baada ya ile gharika, Muumbaji aliongeza nyama ya wanyama "safi" katika lishe yao (Mwanzo 7:2-3, 9:1-6)
(Mwanzo 3:18). Baada ya ile gharika, Muumbaji aliongeza nyama ya wanyama "safi" katika lishe yao (Mwanzo 7:2-3, 9:1-6)
Nyama
ya wanyama ina mafuta ya majimaji (saturated fat) na mafuta mazito kolestero
[cholesterol], ambayo yote huongeza hatari ya kupatwa na shinikizo la
damu, kupooza (stroke), ugonjwa wa moyo, kansa, unene usio wa kawaida,
kisukari na magonjwa mengineyo. Leo matabibu wengi wanawashauri wale
wanaokula nyama kula mnofu ule tu usiokuwa na mafuta, uliopikwa vizuri,
pamoja na kula samaki na kufanya hivyo kwa nadra sana.
Kwa
vile watu wanaokula chakula cha mimea wana afya bora zaidi, tena wanaishi
kwa muda mrefu zaidi, wataalamu wengi wa lishe na afya wanatusihi sana
sisi ili tupate kufikiria kukirudia chakula kile cha awali walichopewa
wanadamu cha kokwa, nafaka na matunda pamoja na mboga za majani zilizoongezwa.
Ukitaka
kuanza kula vyakula vya mimea, hakikisha kwamba unaelewa kwanza namna
ya kuandaa lishe bora bila kutumia nyama. Ule kiasi cha chakula kinachomtosha
mtu kula kwa siku (migawo [serving] mitano au sita hivi) ya aina mbalimbali
za matunda, pamoja na kokwa [karanga n.k.] nafaka, maharage, kunde,
mbaazi na mboga za majani. Mboga za majani za kijani na za njano, pamoja
na machungwa ni za muhimu sana. Tumia unga wa nafaka isiyokobolewa na
mchele mwekundu (brown rice) badala ya ule mweupe. Ulaji wako wa wanga
na sukari za mchanganyiko ungekuwa katika migawo (servings) sita au
zaidi kwa siku moja. Badilisha matumizi yako ya mafuta ya wanyama (samli,
siagi, mafuta ya nguruwe, shahamu izungukayo figo, n.k.) kwa kutumia
mafuta ya mimea. Lishe hiyo juu inatosha bila kutumia nyama kama wewe
unatumia vitu vinavyotokana na maziwa.
Wale
wanaochagua kula nyama kama sehemu ya chakula chao, wangepaswa kuzila
nyama zile tu ambazo Biblia inasema ni "safi"au zile zinazofaa
kuliwa na wanadamu. Mungu alipowaruhusu wanadamu kula nyama baada ya
gharika (Mwanzo 7:2-3) (Mambo ya walaei 14:47), alibainisha nyama za
wanyama gani zilikuwa safi, na zipi zilikuwa najisi na zilikuwa hazifai
kuliwa.
Soma
katika Mambo ya Walawi 11 na Kumbukumbu la Torati 14 orodha ya ndege,
wanyama, na samaki ambao Mungu alisema hawafai kuliwa. Kwa mujibu wa
sura hizo, wanyama safi ni lazima kwato zao zigawanyike na pia wacheue.
Samaki safi ni lazima wawe na magamba na mapezi, vyote viwili. Ndege
wanaokula uchafu ni marufuku kuliwa.
Miongoni
mwa wanyama najisi, kwa namna ya pekee nguruwe wanatajwa kwa kulaaniwa
(Kumbukumbu la Torati 14:8) Asilimia ya juu ya miili ya wanadamu inayofanyiwa
uchunguzi na waganga imejaa minyoo isiyokufa ya trikina (trichinae).
Minyoo hiyo midogo sana inahamishiwa kwa wanadamu wale wanaokula nguruwe
walioambukizwa minyoo hiyo. Utafiti wa kisanyansi wa siku hizi unazidi
kufunua sababu zinazoonyesha kwa nini Mungu alitangaza nyama za wanyama
fulani kuwa ni najisi. Sababu moja huenda ikawa ni yale matokeo yanayoleta
uharibifu mkubwa kutokana na mafuta ya wanyama ya majimaji katika mfumo
wa mwili wa kibinadamu wa kuyeyusha chakula.
7.
Epuka Vitu Vinavyoleta Madhara
Je,
ni maonyo gani ambayo Biblia inatoa kuhusu vinywaji vyenye alcohol ndani
yake?
"Mvinyo hudhihaki na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima" - Mithali 20:1
"Mvinyo hudhihaki na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima" - Mithali 20:1
Wala
wezi wala watamanio, wala WALEVI, wala watukanaji hawataurithi ufalme
wa Mungu" - (1 Wakorontho 6:10).
Alkoholi
huathiri mifumo ya mwili ifuatayo:
1. Mfumo wa kinga mwilini - Alkoholi inapunguza uwezo wa chembechembe nyeupe wa kupigana na ugonjwa, hivyo kuzidisha hatari ya kupatwa na nimonia (pneumonia), kifua kikuu, homa ya manjano, na kansa za aina kadhaa.
2. Mfumo wa tezi (endocrinesystem) zinazotoa majimaji mwilini - Vinywaji viwili tu au vitatu kwa siku huzidisha hatari ya kuharibika mimba, kuzaa watoto waliokufa, na watoto waliozaliwa kabla ya wakati wake.
3. Mfumo wa mzunguko wa damu mwilini Matumizi ya alkoholi huzidisha hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo, hupunguza sukari katika damu, na kuzidisha kiwango cha mafuta katika damu na kuongeza mapigo ya moyo, hivyo kuzidisha shinikizo la damu.
4. Mfumo wa kuyeyusha chakula - Alkoholi inaleta kuwasha tumboni, na kwa njia hiyo kusababisha kutoka damu katika tumbo hilo… Mazoea ya kutumia alkoholi huzidisha hatari kwa ini kuw ana mafuta mengi, homa ya manjano, na ugonjwa wa ini (cirrhosis).

inahusika na asilimia kubwa ya watu wanaojiua wenyewe, vifo vinavyosababishwa
na magari, kuwatendea vibaya watoto, na ukatili uliomo nyumbani.
8.
Kuutumainia Uweza Wa Mungu
Mtu anayesumbuliwa mara kwa mara na hofu au hatia ataona vigumu kwake kupata manufaa kamili kutokana na mazoea hayo ya afya tuliyotoka kuyaeleza muda mfupi tu uliopita. Lakini mtu yule mwenye imani isiyo na shaka kwa Mungu atapata chimbuko hili la mwisho litakalomletea hali njema katika maisha yake.

"Ee
nafsi yangu umhimidi BWANA, wala usizisahau fadhili zake zote - yeye
anayekusamehe dhambi zako zote na KUKUPONYA MAGONJWA YAKO YOTE, ANAYEUKOMBOA
UHAI WAKO na kaburi" - Zaburi 103:2-4.
David
Larson, mshauri wa Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akiliki kule Marekani,
alifanya utafiti wake mpana juu ya uhusiano wa moja kwa moja uliopo
kati ya dini na afya.Uchunguzi wake ulionyesha wazi kwamba upo uhusiano
wa moja kwa moja kati ya Mkristo aliyejitoa na afya. Alishangaa kujua
kwamba, wale wanaohudhuria kanisani wanaishi kwa muda mrefu kuliko wale
wasiohudhuria. Wale wanaokwenda kanisani wana upungufu wa kupatwa na
mshtuko wa moyo, Mishipa ya arteri kuwa migumu, shinikizo la damu, na
magonjwa mengine. Wale wanaomwamini Mungu huishi maisha yenye manufaa
zaidi kwa sababu hawapatwi kirahisi na mfadhaiko, hawageuki na kuwa
walevi sugu, kufungwa kama wahalifu wanaorudia mle tena na tena, na
kunaswa katika ndoa isiyo na furaha. Kuutamainia uweza wa Mungu ndio
msingi wa ustawi wa kweli na maisha ya afya yenye furaha.
Waadventista,
Wasabato wapatao 50,000 hivi walichunguzwa, hasa kule California kwa
kipindi cha zaidi ya miaka 30. Matokeo yalionyesha kwamba Waadventista
wanaume wanaishi miaka 8.9 na wanawake miaka 7.5 kuliko
watu wengine wote kwa jumla. Uchunguzi huo wa Waadventista kule Uholanzi, Norway na Polandi huonyesha matokeo yanayofanana na hayo. Watafiti wanaona kwamba sababu ya kipindi kirefu cha kuishi kwa Waadventista inatokana na kuzifuata kwao baadhi au kanuni zote nane za afya zilizoelezwa katika mwongozo huu. Wale wanaozifuata kanuni hizi sio tu kwamba wana maisha marefu zaidi, bali pia wana maisha yaliyo bora sana.

Tukiutumia
mtazamo wa Biblia katika maisha yetu tutakuwa tofauti katika aina zote
za njia za utendaji wetu na kutoa ushahidi unaovutia kuonyesha kwamba
katika ulimwengu mzima Ukristo ni dini inayoweza kuwekwa katika vitendo.
Inawabadilisha watu - yaani, fikra zao na matendo yao na kujenga mtindo
mpya wa maisha.
Kutokana
na uhusiano wa karibu sana uliopo kati ya akili, mwili na maisha yetu
ya kiroho, Wakristo wale wanaoishi kwa Neno la Mungu watataka kuzifuata
kanuni hizo za mtindo wa maisha uletao afya wanapojiandaa kwa ajili
ya marejeo yake Yesu (1 Yohana 3: 1-3). Sio tu kwamba Kristo anataka
sisi tuwe tayari kukutana naye atakaporudi, pia anataka kuyaboresha
maisha yetu ya sasa. Tunaweza kushirikiana naye kwa kuzifuata hizo kanuni
za afya za Mungu.
Yesu
anaahidi kutuokoa sisi mbali na kila tabia iletayo uharibifu mwilini
kwa " kadri ya nguvu [yake] itendayo kazi ndani yetu" (Waefeso
3:20). Endapo wewe unajitahidi kuishinda tabia fulani inayokuathiri
mwili wako kama vile kutumia tumbaku au kunywa vileo, basi, maazimio
yako hayo mazuri sana ya kutaka kuacha tabia hiyo mara nyingi yanageuka
na kuwa kwako kama kamba za mchanga. Lakini kwa kuuchota uwezo wa Mungu
unaotenda kazi ndani yako Mungu aweze kukupa wewe nguvu za kukuwezesha
kushinda. Neno la Mungu linaahidi hivi: " Naweza kufanya mambo
yote kwa njia yake Kristo anitiaye nguvu" (Wafilipi 4:13)