Wataalamu
wa afya wamethibitisha kuwa saratani ni janga la kitaifa huku takwimu
zaidi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo zikionyesha Watanzania wengi
hupoteza maisha kila siku.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ocean Road Dk. Diwani Msemo wakati
wa maazimisho ya siku ya saratani duniani alisema wengi wanaopata
ugonjwa huo hufa kwa sababu wanakosa tiba, uhaba wa dawa na vifaatiba na
pia wanachelewa kugundua iwapo wana ugonjwa huo.
Takwimu zilizoandikwa kwnye gazeti la Mwananchi zinaonyesha kuwa watu kati ya 80 hadi 100 hufariki kila siku.
Waziri wa afya Dk. Seif Rashid alisema asilimia 10 tu ndio wanaofika kutibiwa huku asilimia 80 wakiwa katika hatua za mwisho za ugonjwa huo.
Takwimu
za kidunia zinaonyesha kuwa watu 8,000,000 hufa kila mwaka kwa saratani
na hapa nchini watu 27,000 hufa kila mwaka huku 35,000 hugundulika ni
wagonjwa.