Katika baadhi ya sehemu duniani watu
wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria
uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao
mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye
ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini
ya kiwango,
hii hupelekea watu hawa kutumia ving
´arisha ngozi kama krimu, vidonge au
nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.
Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na
wasichana hupendelea kutumia bidhaa
zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata
hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na
jamii. Kwa kweli,hata matangazo
yanayoonyeshwa kwenye televisheni
mbalimbali huonyesha kitu hiki. Mambo
hayo yote huwa na athari kubwa juu ya
mawazo ya vijana wa kiume na wakike
ambayo hupelekea kuwafanya wachague
chochote wanachomudu kati ya krimu au
vidonge.
Madhara ya kujichubua ni yapi?
Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa
ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi,
ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa
hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka,
pumu, kupata watoto wenye kasoro,
kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini,
kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja
na figo kutokana na kiwango kikubwa cha
zebaki(mercury) kilichomo katika
krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito
wa mifupa ambapo huongeza hatari ya
kuvunjika kwa mifupa)
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara
moja na mengine hujitokeza kadri mtu
anavyotumia ving´arisha ngozi.
 
Top