Ukweli utokanao na tafiti kuhusu umuhimu wa mazoezi katika
kujikinga na kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.


Habari njema kwa wanaume wenye tabia ya kufanya mazoezi, na sababu
nzuri kwa wale wasiofanya kuanza kufanya mazoezi. Wanaume
wanaofanya mazoezi kwa kati ya masaa matatu mpaka matano kwa wiki
wanauwezekano mdogo wa kupata matatizo ya upungufu wa nguvu za
kiume kuliko wasiofanya kabisa. utaafiti mkubwa iliyofanyika katika chuo
kikuu cha Havard nchini marekani umebaini. Utafiti huo uliojulikana kwa
jina la Havard Health professionals Follow-up Study (HPFS), ulichapisha
matokeo hayo katika jarida la kisayansi linalojulikana kwa jina la ’’Annals
of Internal Medicine`` mwezi wa nane mwaka 2003
Magonjwa ya moyo hujionyesha kwa kupungua kwa nguvu za
kiume.

Mfumo wa moyo na mishipa ya damu ndio unaohusika haswa na nguvu za
kiume. Kitu kingine kinachohusika na nguvu za kiume ni homoni
ijulikanayo kama testosterone, ambayo mara nyingi hujulikana kama
homoni ya kiume. Kwa maana hiyo basi matatizo ya moyo na mishipa ya
damu huanza kujionyesha mapema kama upungufu wa nguvu za kiume.
Kushuka kwa kiwango cha homoni ya testosterone ambacho hutokea
kadiri umri unavyoongezeka pia huchangia kusababisha upungufu wa
nguvu za kiume. Mazoezi, hususani kutembea, kukimbia, kuendesha
baiskeli na mazoezi mengine yanayoufanyisha moyo kazi hupunguza
uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo na hivyo kusaidia mzunguko
wa damu. Mazoezi pia husaidia kuongeza kiasi cha homoni testosterone.

Wanaume wangi wako kwenye hatari ya kupata upungufu wa
nguvu za kiume.
Utafiti mkubwa uliohusisha zaidi ya wanaume 31,000 ambao hawakuwa
na saratani ya tezi ya prostate (prostate cancer), ulionyesha kwamba
theluthi moja ya wanaume hao waliwahi kupata upungufu wa nguvu za
kiume. Uwezekano wa tatizo hili unaongezeka kadiri umri
unavyoongezeka. Utafiti huu pia ulionyesha kwamba, mazoezi yanaweza
kuongeza muda wa mwanaume wa kawaida kuendelea kuwa na nguvu za
kawaida za kiume kwa zaidi ya miaka kumi. Tafiti zilizopita zimeonyesha
mazoezi yanaweza pia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi
ya prostate, ambayo matibabu yake huweza kusababisha kupoteza nguvu
za kiume.

Sababu zingine zinazoweza kusababisha kupungukiwa kwa nguvu
za kiume.
Tofauti na kutokufanya mazoezi, sababu zingine zinazoweza kubadilishwa
ambazo pia huongeza uwezekano wa kupungukiwa kwa nguvu za kiume ni
pamoja na uvutaji sigara, na unene uliokithiri. Kujenga tabia ya kufanya
mazoezi mara kwa mara na kula chakula bora kunaweza kusaidia kwa
kiasi kikubwa sana katika kujikinga na tatizo hili.
Ni wakati muafaka wa kuchukua uamuzi na kujenga tabia ya kufanya
mazoezi, na kula chakula bora.

 
Top