Pre mature ejaculation ni nini?
Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa kumridhisha mpenzi wake.
Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada ya hali hii kutokea.
Kimsingi mwanaume anatakiwa achukue dakika nne mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.
Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}
Chanzo ni nini?
Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.
· Kupiga punyeto haraka kipindi cha kubalehe kuogopa kukutwa na watu.
· Kukaa mda mrefu sana bila kushiriki tendo la ngono.
· Kuwa na wasiwasi kipindi cha tendo la ndoa kwamba huenda mwanamke anaweza akavaa akaondoka kabla hujaridhika.
· Madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu.
· Kurithi tatizo kwenye ukoo. I;e genetically inherited.
· Magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwanaume mfano prostatitis.
Diagnosis{ kuutambua ugonjwa]
Mwanaume yeyote ambaye anatoa mbegu chini ya dakika moja ni muhanga wa hili tatizo na anatakiwa apewe matibabu.
Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyika sehemu kuu mbili kulingana na ukali wa tatizo husika.
· Non pharmacological treatment{matibabu yasiyo hitaji dawa}: matibabu haya hupewa watu ambao wanahimili mpaka dakika tatu bila kutoa mbegu.
· Pharmacological treatment{matibabu yanayohusu dawa}: matibabu haya hupewa watu ambao hutoa mbegu ndani ya dakika moja baada ya kuanza kushiriki tendo la ndoa, watu hawa hushauriwa kutumia na mbinu zote mbili za matibabu.
Yafuatayo ni matibabu yasiyohitaji dawa.
· Tumia condom:
Condom ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hili kwani hufanya kazi kwa kupunguza hisia kali za mapenzi mtu anazozipata pale ambapo hatumii condom.
· Kandamiza perineum kwa kidole:Perineum ni eneo kati ya mkundu na korodani, ile sehemu ikikandamizwa na kidole huweza kuzuia kukojoa haraka
.
· Punguza wasiwasi: hebu lifikirie tendo hili kama njia ya kujifurahisha sio njia pekee ya kutafuta kutoa mbegu, hii itakusaidia kuondoa mawazo ya kutafuta mbegu na kuchelewa kumaliza.
· Fanya taratibu: picha za ngono zinadanganya sana watu kwamba kulala na mwanamke lazima ufanye kwa haraka haraka kama bata. HAPANA; ukifanya taratibu ndio njia nzuri ya kumfikisha mwenzako na wewe kuchelewa kufika kileleni.
· Badilisha style: ile style ya zamani ya kumlalia mwanamke kwa juu{missionary position} inaleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uuume hivyo itakufanya ufike haraka sana.
· Tumia style ya wewe mwanaume kutangulia chini afu mwanamke juu au kulala kwa upande wote mnaangalia upande mmoja hii itakusaidia sana kuchelewa
· Toa mawazo kwamba unafanya ngono: hebu jaribu kufikiria mambo mengine ya kikazi au masomo wakati unafanya tendo hilo, hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi na kuchelewa kufika.
· Fanya na kuacha: hii ni ile hali ya kuzuia msuguano pale unapoona unakaribia kutoa mbegu kwa kama sekundi 30 kisha unaanza upya. Hakikisha haufiki “point of no return”. pointi ambayo huwezi kujizuia tena kumaliza.
· Kandamiza sehemu ya shingo la uume: hii sehemu ya shingo ya uume kwa chini ambayo ukiibana itakusaidia kuanza upya tena kihisia. Nimetumia shingo la uume kwasababu najua uume hauna mabega.
tumia kilevi: unywaji wa pombe mfano bia mbili kwa siku kwa wanaume au bia moja kwa siku kwa wanawake unasidia sana mfumo wa moyo lakini sio bia tu hata wine, whisky au kilevi chochote kwa kiwango kidogo kama glass moja kwa siku..pamoja na faida ya moyo, pombe hupunguza kidogo nguvu ya mishipa ya fahamu na kufanya mtu aliyekunywa kuchelewa sana kufika kileleni, [watu wanaokunywa pombe lazima mtakubaliana na hili] hivyo unaweza kunywa bia, wine au whisky nusu saa kabla ya tendo na kuondoa shida hii.
·
Matibabu ya kutumia dawa.
1. Serotonin reuptake inhibitors mfano paroxetine na clomipramine zimefanya kazi nzuri ya kuzuia mara 20 zaidi kutoa mbegu zikitumika vizuri.
2. anesthetic creams: hii hupakwa kwenye kichwa cha uume na huzuia msisimuko ni moja ya dawa nzuri sana wakati wa tendo la ndoa.
mwisho: shida hii inaathiri sana watu wanokaa muda mrefu sana bila kushiriki kingono, nakushauri utumie pombe au dawa kama ukijikuta umekaa mda mrefu sana bila kushiriki ngono lakini kama hua unalala na mwanamke angalau mara nne kwa wiki huhitaji dawa wala pombe kwani tatizo kwako litapungua sana
Home
»
AFYA
»
AFYA YA UZAZI
» KAMA WEWE MWANAUME UNA TATIZO LA KUFIKA KILELENI HARAKA KABLA MPENZI WAKO HAJARIDHIKA SOMA HAPA