Utafiti
uliofanywa wataalamu wa masuala ya jinsia umeonyesha kwamba kuna mfanano katika hali ya
ubongo hususani katika eneo liitwalo hypothalamus
kwa wanaume ambao ni mashoga “gay males”
na wanawake, sehemu hizi katika ubongo kwa mashoga na wanawake ni kubwa kuliko
kwa wanaume wakawaida “straight males”.
Ukubwa wa eneo hili katika ubongo unaaminiwa pia kuchangia katika tofauti za
kijinsia, tofauti za uwezo wakiakili na uwezo wa lugha au kuzungumza. Na hii
ndiyo inayosababisha watafiti wengi kulinganisha uwezo mkubwa wa kuongea “verbal abilities” walionao wanawake na wanaume
mashoga “gay males”. Hata hivyo zipo
tafiti zilizoongeza kwamba kuna maeneo mengine pia katika ubongo wa mwanaume wa
kawaida na mwanaume shoga yanayotofautiana kabisa kwenye mvuto wa kimapenzi.
Tafiti hizi zinaonyesha kwamba eneo linalohusika na mvuto wa kimapenzi katika
ubongo wa mwanaume shoga huhemshwa au kustuliwa na harufu ya jasho la mwanaume
mwenzake wakati hali hii haipo kwa mwanaume wa kawaida.Tafiti hizi
zimehitimisha kwamba asilimia 35 ya sababu za mwanaume kuwa au kutokuwa shoga,
na mwanamke kuwa msagaji “lesbian” au
kutokuwa msagaji husababishwa zaidi na vinasaba “genes” na hizo asilimia 65 zilizobaki hazijapatiwa uhakika wa
kisayansi ingawa mazingira yanatajwa zaidi kuhusika.
CREDIT:
www.chrismauki.com