Habari za leo Alhamis ya leo Septemba 10, 2015 mdau wa www.dkmandai.com bila shaka umzima wa afya tele karibu tufahamishane mengine haya kuhusu afya zetu.

1. Hakikisha haya matatu unayazingatia, kula vizuri, kufanya mazoezi ya kutosha na kupata nafasi ya kupumzika vizuri.

2. Dumisha hali ya usafi katika mazingira unayoishi kwa kuhakikisha unanawa mikono kabla ya kula na mara baada ya kutoka chooni

3. Hakikisha chakula unachokula wewe na familia yako ni salama kuanzia mazingira ya kuandalia chakula hicho, pia hakikisha unahifadhi chakula vizuri.

4. Jitahidi kupata chanjo kwani husaiida kuimarisha kinga zako na kuzipanguvu zaidi ya kupambana na viini vinavyopatikana mahali unapoishi.
 
Top