Kuna watu wanapata shida sana kutokana na kuwa na uzito mkubwa, jambo ambalo huwakosesha raha pia.

Leo napenda kukufahamisha hizi mbinu za kukabiliana na kuwa na uzito kupita kiasi hebu jaribu kufuata haya yafuatayo:

Tembea kwa nusu saa asubuhi kisha baada ya kukamilisha mazoezi yako tafuta maji ya  uvuguvugu kunywa glasi  mbili hadi nne

Jitahidi  kunywa supu ya mboga mboga (vegetable soup) pamoja na matunda, huku ukiepuka kula vyakula vyenye mafuta mengi pamoja na kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi pia.

Kuhusu kufanya mazoezi unashauriwa kufanya kabla ya kunywa chai asubuhi. Mazoezi kwa ujumla yana umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu, hasa kama yataambatana na lishe bora. 

Kwani kitendo cha  kufanya mazoezi huweza kuzuia magonjwa sugu kama vile kisukari, magonjwa ya moyo, saratani na shinikizo la damu, ni vyema ikafahamika pia kuwa familia ambazo hufanya mazoezi huwa na afya bora.

Mazoezi pia husaidia sana kuboresha tendo la ndoa na hivyo kuleta amani na mahusiano mazuri ndani ya familia kwani mtu anayefanya mazoezi bila kujalisha ni mazoezi ya aina gani basi kwa kawaida huwa na uimara katika afya.

Hayo ni machache tu kuhusu mada hii ya kupunguza uzito endelea kuwa karibu na tovuti hii ili kuyapata mengine mengi kuhusu mada hii, lakini kama utakuwa na ushauri, maoni unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 
0784 778788
 
Top