Mimi naitwa Isaack ni kijana mwenye miaka 28, nimeoa. Nimekuwa na mazoea ya kupiga punyeto kuanzia mwaka 2007 nikiwa mwaka wa kwanza chuo kikuu baada ya kuanza kuangalia picha za ngono. Licha ya kwamba nimeoa lakini naona kama siwezi kuacha mchezo huu. Nimekuwa nikisikia watu wakisema vijiweni kuwa mtu anayefanya masterbation anaweza kupoteza nguvu za kiume au kushindwa kumridhisha mke. Nikisikia stori hizo huwa naingiwa na hofu. Kwa sasa  sina tatizo lolote na shemeji yenu anapata haki yake kama kawaida. Je nini madhara ya punyeto kama nitaendelea kwa muda mrefu?

 
Top