Habari za leo ndugu msomaji wa blog hii ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia blog yangu hata hvyo iwapo una maoni au chochote unaweza kuwasiliana Nami kupitia namba Zangu 0625 539100 , leo nazungumzia tatizo la wamama na wasichana kukosa hedhi kwa muda Hali ambayo huwaweka katika mazingira mabaya na kuwaharibu kiakil, tatizo hili kitaalamu linajulikana kama (AMENORRHEA)
AMENORRHEA ~hii ni hali ya mwanamke ambaye amepevuka na kukomaa maumbile yake ya Uzaz kushindwa kupata siku zake (breed), tatizo hili limekua likiwasumbua na kuwaletea usumbufu wa kisaikolojia wanawake wengi
~tatizo hili la kutopata hedhi linaweza kutokea awali au baadae kabisa hivyo kuna aina mbili za amenorrhoea
(A) PRIMARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inay
oweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kubalehe ambayo huweza kuendana na kutopata mabadiliko ya kimaumbile yanayotokea kipindi cha kuvunja ungo (kubalehe)kama vile kuota nywele sehemu za siri, kuota matiti Lakini pia hapati hedhi
(B) SECONDARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito wala hanyonyeshi na ambaye hajakoma hedhi (menopause) na wala hatumii dawa za Uzazi wa mpango ambapo pia awali alikua akipata kama Kawaida Lakini akasimama kwa muda
NAMNA AMBAVYO MWANAMKE HUPATA HEDHI
~kwa Kawaida ili mwanamke apate hedhi katika mzunguko uliosawa ni lazima tezi ya hypothalamus na pituitar pamoja na kiwanda cha mayai (ovaries) viwe vinafanya kazi kwa ushirkiano yani sawasawa
VYANZO VYA TATIZO HILI
Vyanzo au visababishi vya tatizo hili vyaweza kuwa katika Makundi matatu ambayo huhusisha mfumo wa homoni, mfumo wa njia ya Uzazi, mfumo wa mabadiliko, Vyanzo hivyo ni
👉matatizo katika hypothalamus ambapo huweza kusababisha matatizo ya mwanamke kukosa hedhi
👉uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitar
👉ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya Uzazi ugonjwa huu hujulikana kama (KALLMAN SYNDROME)
👉lishe Duni na utapiamlo
👉uzito mdogo kuliko Kawaida
👉pituitar kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa hii ni iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua
👉kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu (PROLACTINEMIA)hii prolactin ni homoni inayochangia uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha
👉kuchelewa kukomaa kwa viungo vya Uzazi eg, uke na ovary
👉matumizi ya dawa za Uzazi wa mpango pia ni chanzo cha tatizo hili la kutopata hedhi kutokana na homoni nyingi ya progesterone iliyopo katika dawa hizo eg, DEPO PROVERA
👉msururu wa mawazo
👉ugonjwa wa kurithi wa galactosema unaoambatana na kuwa na kiwango kidogo cha sukari aina ya galactose ktk damu
👉mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa Chakula kwasababu tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika Hali nzuri
👉kuziba kwa utando unaozunguka uke (Hymen) hivyo kukosekana tundu la kupitishia damu (IMPERFORATE HYMEN)
👉baadhi ya magonjwa ya viungo vya Uzazi husababisha kusimama kwa hedhi mfano wa magonjwa hayo ni POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME
👉Menopause (hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 45_60 homoni zinazohusika na kupata siku za hedhi huwa Kwenye kiwango cha chini sana kiasi haziwezi kufanya kazi vizuri
DALILI ZA AMENORRHEA
👉mwanamke kuwa na mhemko kuliko Kawaida
👉mwanamke kuwa mkavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatzo katika ovary
👉matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito wala hanyonyeshi
👉mwanamke kuwa na vinyweleo vingi na kuota ndevu hii inamaanisha na kuashiria kuwepo kwa kwa wingi wa homoni za kiume za ANDROGEN
👉kuongezeka uzito kupita kiasi
MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA KUONDOA TATIZO HILI
matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kutibiwa hospital kutokana na chanzo cha tatizo ambapo huwa ni kupewa dawa au kufanyiwa upasuaj
NOTE :::ni vizuri kuongea na daktari ili ajue ni kwa namna gan atakusaidia pia waweza kufanya mambo yafuatayo kujitibu hili tatizo
👉ZINGATIA ULAJI ULIOSAHIHI AMBAO UNAHUSISHA ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI
👉fanya masaji Kwenye tumbo la chini kwa kutumia maji ya moto kias (uvuguvugu) Hii itasaidia kuongeza damu nyingi kutoka
👉kula Chakula kisichotokana na damu hivyo kula Chakula chenye protin nyingi mfano Nazi, maharage, na karanga
👉tumia juice ya SOY na tikiti maji (watermelon)
KAMA UNASUMBULIWA NA TATIZO HILI ZAIDI USISITE KUNITAFUTA 0625 539100 NITAKUPATIA DAWA ILIYOWASAIDIA WATU WENGI KUONDOA TATIZO HILI