ni baadhi ya maambukizi yanayotokea mara kwa mara kote ulimwenguni, na huwaathiri watu wa kila rika na asili, wanawake kwa wanaume.
Bora tu wewe hufanya ngono, iwe ya baina ya mke na mume, au iwe baina ya wasenge au wasagaji, ama kushiriki katika aina iwayo ya ngono, basi ni vyema kuchukua tahadhari.
Njia moja ni kutumia vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi haya. Kwa mfano kutumia kondom na mpenzio, kila mara mnapofanya ngono, hadi pale nyote wawili mtakapokuwa mna hakika kabisa kwamba hakuna uwezekano wowote wa ninyi wawili kuambukizana magonjwa ya ngono.
Hebu tuangalie orodha hii ya baadhi ya mengine yakuambukuzana kupitia ngono.
Chlamydia -
Husababishwa na viini vya bacteria na waweza kuathiri uke, mrija wa kupitisha mkojo, uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa.
Dalili:
Kwa wanawake dalili hazionekani kwa urahisi. Ubaya ni kuwa ugonjwa huo unaweza kuathiri fallopian tubes – yaani mirija ya kupitia mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye nyumba ya uzazi hivyo basi kusababisha utasa. Wakati mwengine dalili hii unaweza kuiona – kutokwa na majimaji ya ukeni yasiyo ya kawaida na kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.
Kwa wanaume ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitishia mkojo, uzuri ni kwamba dalili huonekana wazi, kama vile uume kutokwa na ute na kusikia maumivu wakati wa kukojoa.
Matibabu:
Ni pamoja na kufanyiwa uchunguzi wa mkojo au damu. Unapotambuliwa daktari hupendekzeza dawa maalum ya kumeza. Kama umefanya mapenzi hivi karibuni basi yafaa mpenzi huyo aarifiwe ili nae atibiwe pia.
Kisonono (Gonorrhoea)
Huu husababishwa pia na bacteria. Unapofanya mapenzi na mtu mwenye kisonono unaweza kuaathiri viungo kama vile uke, uume, sehemu ya haja kubwa na ya haja ndogo, na hata koo au mdomo kama ukifanya mapenzi ya kunyonyana.
Dalili:
Wanawake hutokwa na ute mwingi wa njano au kijani kutoka ukeni na kusikia maumivu wakati wa kukojoa. Kwa wanaume uume uliathirika hutoa ute wa njano au kijani, na kupata maumivu wakati wa kukojoa.
Pia kuna uwezekano wa kuwashwa ama kutokwa na maji maji katika sehemu ya kupitishia haja kubwa. Ingawa hivyo baadhi ya watu hawaoni dalili zozote kabisa lakini bado wanaweza kuwambukiza wanaofanya mapenzi nao.
Matibabu:
Iwapo matibabu hayatapatikana kwa haraka kuna hatari ya mirija ya kupitisha mayai (fallopian tubes) kuharibika na hivyo kusababisha utasa.
Kama una kisonono usifanye tena mapenzi hadi utakapofanyiwa uchunguzi na kupewa madawa ya kutibu ugonjwa. Ni muhimu sana kumfahamisha mpenzio ili nae pia atibiwe.
Herpes Huu husababishwa na aina fulani ya kirusi, kama kile kinachosababisha mafua na vidonda vya mdomoni. Mbali na kusambazwa kupitia ngono pia husambazwa kupitia kufanya mapenzi ya kunyonyana sehemu za siri.
Dalili:
Ni Kupata vidonda ukeni au uumeni mfano wa vile vinavyotokea mdomoni wakati wa homa kali ya mafua.
Matibabu:
Sasa kuna dawa na krimu za kupambana na virusi hivi. Lakini kumbuka hata unapotibiwa virusi vya herpes bado hubaki mwilini mwako na vinaweza kuzusha tena vindonda. Pia kama umja mzito unaweza kumwambukiza mtoto wako, hivyo basi kama una vijidonda ni vyema kumjulisha mkunga wako ama daktari ili upate matibabu yafaayo.
NSU ni herufi zinazotumiwa kuelezea magonjwa ya bacteria yanayoathiri mfereji wa
kupitisha mkojo yaani urethra. Magonjwa hayo husambazwa kwa kupitia
kufanya mapenzi.
Dalili:
Kwa wanaume dalili kubwa ni kutokwa na ute, kutoka kwenye tundu ya uume na huenda akahisi maumivu wakati wa kukojoa. Huenda ukasikia maumivu au kuwashwa-washwa.
Matibabu:
Majimaji yakitoka kwenye uume, isipokuwa mkojo au manii, ni lazima uchunguzwe na daktari, au nesi katika kliniki ya afya ya uzazi. Unaweza kutibiwa kwa kutumia vidonge vya anti-biotics.
Kaswende (Syphilis)
Ugonjwa huu nao husababishwa na bacteria Treponema Pallidum
Dalili zake hazionekani kwa urahisi. Huenda ukaanza kwa kijidonda au kipele kwenye uke au uume au sehemu ya kupitishia haja kubwa. Kidonda hiki kinapopona usidhani ndio mwisho wa maambukizo la! Viini hivyo vinaweza kubaki mwilini kimya kimya kwa miaka mingi!
Matibabu:
Ni bora daktari kufanya uchunguzi wa damu kwani majimaji ya ukeni au uumeni huenda uchunguzi wake usionyeshe viini vya kaswende. Kaswende ni hatari, kama haitibiwi, inaweza kusababisha utasa au ugumba, na hata kuathiri moyo, mishipa ya damu, ngozi ya mwili, mifupa na hata ubongo na kurukwa na akili.
Hata hivyo matibabu yake ni rahisi – Zipo dawa aina (antibiotics) zinazoweza kutibu kaswende kabisa. Ili kuzuia kuenea kwa maradhi hayo ni vyema mpenzio nae pia atibiwe