Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa
kushirikiana na uongozi wa wilaya za Rungwe na kyela wamefanikiwa
kukamata na kuteketeza shehena kubwa ya pombe haramu aina ya viroba,
vipodozi, dawa na vyakula ambavyo muda wake wa matumizi umepita, bidhaa
ambazo zimekamatwa wakati wa operesheni ya kutokomeza uingizwaji wa
pombe haramu za viroba mkoani mbeya.
Shehena ya pombe haramu za viroba, vipodozi, vyakula na dawa ambazo
muda wake wa matumizi umekwisha vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 20 vimeteketezwa kwa nyakati tofauti katika wilaya za rungwe na
kyela, zoezi ambalo limesimamiwa na kamati za ulinzi na usalama za
wilaya hizo.
Mkuu wa idara ya usafi na mazingira wilayani rungwe Dk. Nimroud
kipoza na afisa wa mamlaka ya mapato TRA wilayani kyela Paul Walalaze
wanaelezea madhara ya bishaa hizo kiafya na kiuchumi kwa watanzania.
Baadhi ya vijana ambao wameunda kikundi cha kupambana na pombe
haramu za viroba pamoja na dawa za kulevya katika mpaka wa kasumulu
wilayani kyela wamesema mafanikio yao katika kudhibiti bidhaa hizo
yanatokana na kupata ushirikiano mzuri kutoka serikalini.
Meneja wa mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa (TFDA) kanda ya
nyanda za juu kusini, Rodney Alananga amesema zoezi la kupambana na
bidhaa hizo ni endelevu, hivyo akawataka wale wote wanaojihusisha na
biashara hiyo kuacha ili kuepuka kupata hasara.