Kutapika wakati wa ujauzito
Kutapika
ni dalili inayojitokeza kwa mama mjamzito hasa kipindi cha awali ingawa
tatizo la kutapika au kuhisi kichefuchefu linaweza kutokea katika
maradhi mengine mbali na ujauzito.
Hali ya kutapika kwa mama
mjamzito imegawanyika katika makundi mawili.Kwanza ni kichefuchefu na
kutapika wakati wa kipindi cha mwanzo cha ujauzito ( Early pregnancy) na
pili ni kipindi baada ya hicho cha awali (Late pregnancy).
Tukiingia
kiundani kila kundi limegawanyika katika sehemu mbili.Ingawa hatutazama
ndani zaidi,ila jambo la msingi ni kwamba katika hali ya awali (Early
pregnancy),kutapika na hali ya kichefuchefu inaweza kuwa ya kawaida na
isimletee shida kubwa mama (Morning sickness) na kutapika kidogo (emesis
Gravidarum) na kuwa mgonjwa hata asiweze kufanya shughuli nyingine.
Mama
huumwa hadi kuishiwa maji mwilini kwa kutema mate,kutapika na kushindwa
kula na wakati mwingine hulazwa hospitali, hali hii huitwa kitalaam
“Hyperemesis gravidarum.”
Yapo magonjwa mengine yanayosababisha kichefuchefu na kutapika ambayo yanaweza kumpata mama mjamzito na asiye mjamzito.
Magonjwa
haya ni kama vile minyoo (Intestrial Infestations) maambukizi ya njia
ya mkojo(Urinary Track infections),magonjwa ya ini(Hepatitis),ugonjwa wa
kisukari (pale sukari inapokuwa juu) (Ketoacidosis of Diabetes),mkojo
kuingia katika mfumo wa damu(uraemia),ugonjwa wa kidole tumbo
(Appendicitis),vidonda vya tumbo (peptic ulcer) kuziba kwa tumbo
(Intestnal obstruction) matatizo ya nyonga kifuko cha mayai (Twisted
Ovarian cyst) na uvimbe katika kizazi (uterine fibroid).
Kutapika
kunakoendelea wakati wa ujauzito (late pregnancy) huwa ni muendelezo wa
hali hiyo.Tangu mwanzoni hali ya awali (Early pregnancy) hutokea mimba
inapokuwa chini ya miezi minne lakini hii hali ya pili ‘Late pregnancy
inatokea mimba inapokuwa zaidi ya miezi minne.Hapa mama huendelea tu
kutapika na vilevile inahusiana na dalili za magonjwa mengine kama
dalili za awali za kifafa cha mimba.
CHANZO CHA TATIZO
Mbali na
maradhi mengine yanayohusiana na tatizo hili la kutapika wakati wa
ujauzito,chanzo cha ugonjwa au tatizo hili ni pale mimba inapokuwa
changa hadi baada ya kufikisha kati ya miezi mitatu na minne inakoma au
ina weza kuendelea hadi miezi sita au hadi mama anapojifungua.
Tatizo hili linaweza kutokea katika mimba ya kwanza tu,wengine hutokea ya pili au wengine hutokea mimba zote.
Hali
hii au tatizo hili linaweza kusababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa
cha hormone au kichocheo cha HCG mwilini au Human Chronic Gonadotrophin
ambacho kikizidi kinakuwa sumu na kuanza kuchefua mwilini.
Hali ya kisaikolojia (psychogenic) pia huchangia kuamsha kichefuchefu kwa kutotamani baadhi ya vitu au vyakula au harufu.
Mama
akiwa na hali hii hasa vyakula vya wanga hasa nyakati za usiku,asubuhi
ataamka na njaa na kichefuchefu na kuanza kutapika na kuchoka.
Chakula
cha wanga kama wali na ugali ni muhimu kwani vinatia nguvu na
joto,vilevile uwepo wa vitamini B za kutosha nao husaidia sana.
Tatizo
hili la kichefuchefu na kutapika pia huchangiwa na mzio (Allergies )
mbalimbali na tumbo kutofanya kazi vizuri (Decreased gastric motility).
NINI CHA KUFANYA
Hali
hii ni tatizo sugu kwa baadhi ya akinamama kwani kila wapatapo mimba
inakuwa shida.Tatizo hili linapoanza na ukawahi kumuona Daktari haliwezi
kusumbua kwa kiasi kikubwa.
Mgonjwa atachunguzwa kama ana baadhi
ya maradhi tuliyoyaeleza au kama kuna hitilafu zozote zilizosababishwa
na ugonjwa.Mgonjwa baada ya uchunguzi atapatiwa tiba kadiri daktari
atakavyoona inafaa.
Tiba mojawapo ni kuongezewa maji na dawa zitakazomsaidia kuondoa au kupunguza kasi ya kichefuchefu.
Mgonjwa
akazane kula hasa vyakula vya jamii ya wanga pale hali inapokuwa
nafuu,kunywa maji mengi na mara kwa mara ili hata kama hali hiyo
itajirudia awe salama asisumbuke sana.