Ni
kawaida kwa mwanaadamu aliye mzima kupenda kuwa na mtoto, na kwa namna
ya upekee katika kuumbwa kwa mwanaadamu, hakuna njia nyingine yoyote ile
ambako mtoto anaweza kupatikana bila ya maingiliano ya kimwili baina ya
watu wa jinsia mbili tofauti (ukiachilia mbali instances chache ambapo
mambo ya test tube na artificial insemination hutumika).
Kifupi
ni kwamba, kama mwanamke atataka kubeba ujauzito ni lazima akubali
kuingiliwa, Vivyo hivyo kama mwanaume anataka kumbebesha mwenza wake
ujauzito ni lazima ahakikishe kuwa amemwiligilia mke
Hata
hivyo, licha ya ukweli wa kuwa ili ujauzito upatikane ni lazima kuwe na
kufanya mapenzi, kumekuwa na mkanganyiko sana juu ya tendo hili la
kufanya mapenzi au kutiana kama wengine wanavyosema, pindi inapotokea
mwanamke ameshashika ujauzito.
Je, ni sahihi kufanya mapenzi wakati mwanamke wako ni mjamzito?
Je, ni hadi muda gani kabla ya kujifungua, ambapo mwanamke mjamzito anaweza kuwa anaingiliwa kimwili na mwenza wake?
Kwa maswali haya na mengine kadhaa, hebu twende pamoja mdogo mdogo kama ifuatavyo:-
1). Je, ni sahihi kufanya mapenzi ikiwa mwanamke wako ni mjamzito?
Ndio, hakuna tatizo lolote kwa mwanamke kuendelea kufurahia mapenzi na mumewe au mpenzi wake wakati anapokuwa mjamzito.
Wataalamu
wanaeleza kuwa, ikiwa ujauzito ulioubeba haukupi shida yoyote ile na
unajisikia uko poa, basi hakuna hatari yoyote ile ikiwa utataka kufanya.
Tatizo
pekee ambalo huwa linawakumba wengi wa wanawake wakiwa wajawazito ni
kuwa, huwa wanapoteza hamu ya tendo lenyewe wanapokuwa katika hali hii,
au kushindwa kumudu kutokana na kujisikia uchovu muda mwingi.
Ingawa
pia wapo wanawake ambao wakiwa katika hali hii ndio kwanza, wanakuwa
wanajisikia kukereketwa huko kwenye ki**i kupita maelezo, na wanatamani
muda wote wafanye mapenzi.
Wapo
baadhi ya wanawake ambao wanakuwa wako normal kimwili, lakini
kisaikolojia wanakuwa na ile hofu ya kuwa kufanya kunaweza kuwaharibia
mimba zao, fikra ambazo huwatoa kabisa katika mstari wa kufurahia tendo
hili.
(2). Je, kufanya wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha ujauzito kuharibika?
Hili pia ni miongoni mwa maswali na hali ambazo zimekuwa zikiwachanganya watu wengi, waume kwa wanawake.
Ila ukweli ni kwamba, kufanya hakuhusiani na kuharibika kwa mimba au kujifungua kabla ya wakati muafaka.
Kwa
kawaida, kuharibika kwa mimba hutokana na sababu zingine tofauti
kabisa, ikiwa ni pamoja na kizazi cha mwanamke kuwa na matatizo hasa
katika kuhimili ukuaji wa kiumbe tumboni na sababu zingine za
kimazingira.
Wala sio kwa sababu ya kitu ambacho unakifanya au hukifanyi.
(3). Je, kufanya wakati wa ujauzito kunaharibu au kumdhuru mtoto?
Kiumbe kilicho tumboni wakati wa ujauzito huwa kinakingwa na ute maalum unaojulikana kitaalamu kwa jina la "amniotic fluid" ndani ya mji wa uzazi, pamoja na kuta za mji wenyewe wa uzazi.
Hakuna
namna ambavyo muhogo unaweza kupita na kufika mahali mtoto anapokuwa
anakua huko ndani, au zile mbegu kuwa zitapita moja kwa moja na kwenda
kumdhuru mtoto.
Kumekuwa
na ule msemo wa kuwa kufanya wakati wa ujauzito ni kulea mimba, watu
wakiamini kuwa mbegu huwa zinakwenda moja kwa moja kwenye kiumbe.
Dhana hii ni potofu. Kama kilivyo chakula cha kawaida mtu anapokula, ndivyo ambavyo mbegu nazo huwa hivyo.
Kila
kitu kwanza lazima kiingie katika mfumo wa kawaida wa usafirishaji wa
virutubisho vilivyo sahihi kuelekea kwenye kiumbe husika.
Hii
ikimaanisha kuwa mbegu nazo huingia katika mfumo huo huo, huchujwa na
kile kinachoonekana kuwa ni kirutubisho kitasafirishwa kwenda kulea
kiumbe, ilhali yale makapi lazima yatatoka.
Tofauti pekee hapa ni kuwa, "mbegu
za kiume zina protini nyingi", hii ikimaanisha kuwa sehemu kubwa ya
kile kinachomwagwa kwenye uke wa mjamzito, kina nafasi ya kutumika kwa
ajili ya kuongeza rutuba kwa kiumbe kinachokuaa ndani ya tumbo.
Na nyingine zinaweza kutoka tu zenyewe bila matatizo yo yote.
(4). Ni mikao ipi (staili) ambayo ni mizuri zaidi kuitumia kufanya wakati wa ujauzito?
Hakuna mkao maalum. Ujauzito sio ulemavu kwamba mnalazimika kujipanga upya namna ya kuridhishana, wala sio ugonjwa pia.
Ikiwa
mwanamke unajihisi uko fresh kuendelea kutumia staili ya mwanzo ambayo
mlikuwa mnaitumia na unafikishwa na mwenzio, huku huyo mwenzio naye
akiwa yuko ok kuitumia staili hiyo na anaimudu hata unapokuwa na tumbo
lako, hakuna shida
Jichumishe mboga, jifanye mbuzi ulogoma kwenda, jifanye namna yoyote ile unayoona uko poa, na mambo yatakuwa vizuri.
(5). Vipi kuhusu kitu ule mtandao wetu na or*l s*x? (chumvi)
Or*l
s*x ni salama kabisa wakati wa ujauzito. Hata hivyo, ni muhimu kuepuka
hewa kuingia ndani ya uke wako wakati ukiwa katika hali hii.
Wapo wale watu watundu ambao hugeuza uke kama pulizo na kujitia umahiri wa kutaka kulijaza hewa wakati wa kupeana raha.
Katika
mazingira ya kawaida, ikiwa mnafurahia hili, hakuna tatizo, ila wakati
wa ujauzito, hii ni hatari kwani inaweza kuleta madhara katika mishipa
fulani ndani ya uke, ambayo iko na uhusiano na mishipa ya kuelekea
kwenye mji wa uzazi.
Kuhusu
ule mtandao wa vijana (Tigo), ambao kwa kawaida hauruhusiwi kutumika,
hakuna wakati unaokuwa mbaya zaidi kuutumia kama wakati huu wa ujauzito.
Katika
wakati huu, uke wa mwanamke mara nyingi unakuwa sensitive zaidi ya
wakati akiwa hana ujauzito, na kuendekeza kuf**ana, kunaongeza hatari ya
bakteria kuhamia kwenye uke na kusababisha magonjwa ambayo yatadhuru
kiumbe kilichobebwa ndani.
(6). Kuna umuhimu wa kutumia kondomu?
Kama nilivyodokeza hapo awali, wakati wa ujauzito uchi wa mwanamke unakuwa sensitive zaidi kwa magonjwa.
Unaweza
tu kuguswa na mwenzako ambaye hakuwa amenawa mikono uzuri na
ikakusababishia tatizo fulani, hivyo basi, inashauriwa kutumia kondomu
ikiwa:
- mwenza wako aliwahi au ana maradhi ya maambukizi
- uko kwenye mahusiano na zaidi ya mtu mmoja
- umeamua kungonoka na king'asti kipya wakati wa ujauzito
Hapana.
Licha ya ukweli kuwa wakati wa ujauzito uke huzalisha kemikali ambazo
ni mahususi kwa ajili ya kumkinga mjamzito na uvamizi wa bakteria wowote
wanaoweza kuwa tishio kwa ujauzito wake, na kwamba kemikali hizi wakati
mwingine huweza kuhitilafiana na lile bao analopiga mwanamke na hivyo
kumletea hali fulani ya kukwaza, kwa ujumla wake hakuna baya linaloweza
kusababishwa na kukojoa au kufika kileleni .
Na wala kufanyana hakuwezi kuathiri kwa namna yoyote ile muda wako wa kujifungua (kuuchelewesha au kuuwahisha)
(8). Je, ni wakati gani mwanamke mjamzito anatakiwa kuacha kufanya mapenzi?
Ijapokuwa
wapo wanawake wengi ambao wanaweza kabisa kuendelea kufurahia kufanywa
hadi siku wanakwenda kujifungua , kuna baadhi ya nyakati mshauri wako wa
afya anaweza kukushauri kuacha ngono kutokana na moja au yote kati ya
yafuatayo:
- umekuwa na tatizo la kujifungua kabla ya muda muafaka kabla ya ujauzito ulio nao
- umetokewa na tatizo la kutokwa na damu kwenye uke
- umekuwa ukitokwa na ute fulani ambao wataalamu wanauita kwa jina la "amniotic fluid"
- umekuwa na tatizo la kwenye mlango wa uzazi, ambalo kitaalamu linajulikana kama cervical incompetence
- kondo la nyuma limesambaa na kuziba kabisa mlango wa uzazi na kuanza kujitokeza kwa nje (placenta previa)
(9). Je, kuna tatizo lolote ikiwa huhitaji kufanya?
Hapana,
na hii ni hali ya kawaida sana kwa baadhi ya wanawake wanapokuwa
wajawazito, ama kutokana na hofu inayokuwa vichwani mwao kuwa atapata
madhara kwa kufanya hivyo, au kutokana tu na aina ya homoni
zinazozalishwa mwilini wakati huo.
Kuna
mengi mnaweza kufanya bila kuhusisha maingiliano ya kimwili na ambayo
yanaweza kumfanya mwanamke kuridhika anapokuwa katika hali hiyo.
(10). Ni baada ya muda gani toka kujifungua mwanamke anaweza kuendelea kufanya mapenzi?
Iwe
kwa njia ya upasuaji au kwa njia ya kawaida, inaeleweka wazi kuwa baada
ya kujifungua, mwanamke anakuwa na hali fulani ya mwili kuchoka, hali
ambayo ni ya kawaida.
Ingawa
wapo ambao wanaweza kujihisi wanamudu kushiriki tendo la ndoa kabla,
lakini wataalamu wanashauri kuwa wakati mzuri wa kurejea kufanyana na
mwenzio baada ya kujifungua, inakuwa ni baada ya kupita wiki sita.