SERIKALI
imesema gharama za kutibu mgonjwa wa kisukari kwa mwaka hapa nchini ni
sh.408,000 na kuwa watu wengi wamekuwa wakiugua ugonjwa huo bila ya wao
kujitambua.


Imeelezwa
kuwa utafiti uliofanya mwaka 2012 katika wilaya 50 nchini ulionyesha ya
kuwa asilimia 9.1 ya watu huugua ugonjwa huo bila wenyewe kujua.


Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Naibu Waziri wa Afya Kebwe
Stephen wakati akitoa tamko la serikali kuhusu siku ya ugonjwa huo
ambayo itaadhimishwa duniani kote kesho alisema ugonjwa huo umekuwa na
changamoto kubwa kwa vile hutokana na ulaji usiofaa.


Alisema
takwimu zinaonesha kuwa watoto wenye kisukari mwaka huu 2014 ni kati ya
asilimia 15 mpaka 20 ya wagonjwa wote kisukari ambao wanatibiwa kwenye
kliniki nchini.


"Maadhimisho
ya siku ya kisukari yataadhimishwa katika  hospitali zote za Rufaa,
mikoa na ngazi  za wilaya kwa wananchi wote  kupima bure sanjari na
kupata dawa,"alisema Kebwe.


Alisema watu wengine wanakuwa na dalili lakini huwa hawachukui hatua za mapema ili kuweza kuuzia ugonjwa huo kuendelea.

Alisema
dalili za ugonjwa wa kisukari ni rahisi kuzitambua nazo ni kusikia njaa
kila wakati,kukojoa mara kwa mara,kupungua uzito, na mwili kukosa
nguvu. 


Kauli
mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani mwaka 2014 ni "Ulaji
unaofaa, huanza na mlo wa asubuhi" na kuwa kauli mbiu hiyo inalenga
kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya ulaji unaofaa ili kuepuka
matatizo mbalimbali yanyotokana na ugonjwa wa kisukari katika jamii. 


 Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Kebwe Stephen (kulia), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo
mchana , wakati akitoa tamko la serikali kuhusu Siku ya Kisukari Duniani
itakayoadhimishwa duniani kesho. 

 Main Symptoms of Diabetes FikraPevu.com

Kama wewe ni mnene kupita kiasi, hufanyi mazoezi kwa ukawaida au una watu wa ukoo walio na kisukari, huenda tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Ongezeko la sukari kwenye damu mbali na kuwa kisababishi cha kisukari, hali hiyo inahusianishwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa akili uitwao 'DEMENTIA'.
Kula sukari nyingi sio sababu ya ugonjwa wa kisukari. Lakini lazima tuseme kwamba kula sukari nyingi si nzuri kwa afya yako kwani utaongeza uzito wa kuweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi tofauti. Ugonjwa wa kisukari umeitwa kwa kufaa "ugonjwa unaoathiri kiini cha nishati ya mwili". Mwili unaposhindwa kutumia glukosi, mifumo mbalimbali ya mwili inaweza kuacha kufanya kazi au hata kusababisha kifo.
Ugonjwa wa Kisukari kitaalamu hujulikana kama 'DIABETES MELLITUS'. Jina 'Diabetes Mellitus' linatokana na neno la Kigiriki linalomaanisha 'kunyonya' na neno la Kilatini linalomaanisha 'tamu kama asali'. Maneno hayo yanafafanua vizuri sana ugonjwa huo, kwani maji hupita mwilini mwa mtu aliye na ugonjwa wa kisukari kana kwamba yananyonywa na mdomo na kupitia kwenye njia ya mkojo kisha kutoka nje ya mwili. Isitoshe mkojo huwa na ladha tamu kwa kuwa una sukari. Ndiyo sababu kabla ya kuvumbua njia bora za kupima ugonjwa huo, mbinu moja ya kutambua kama mtu ana ugonjwa wa kisukari ilikuwa kumwaga mkojo wa mgonjwa karibu na kichuguu cha sisimizi. Ikiwa sisimizi wangevutiwa na mkojo huo basi hilo lilimaanisha kwamba mkojo una sukari.
NI NANI ANAWEZA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI?
Watu walio katika makundi yafuatayo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kisukari:-
– Wenye uzito uliozidi,
– Wenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari katika familia zao,
– Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,
– Watu wasiojishughirisha au wasiofanya mazoezi,
– Wenye shinikizo la damu,
– Wenye msongo wa mawazo na
– Wenye matumizi makubwa ya pombe na sigara.
Watu hawa wanashauriwa kupima sukari yao kila mwaka wakiwa na umri wa miaka 45 na kuendelea.
Kuna hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huo ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu.
Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi kwani zoea hilo hudhuru moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu. Kitabu kimoja kinasema kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
~ Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.
~ Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani.
~ Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
~ Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
~ Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
~ Wanawake kuwashwa ukeni.
~ Kutoona vizuri.
~ Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
~ Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole.
~ Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
~ Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.
~ Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
~ Majipu mwilini.
 
Top