Utafiti uliochapishwa na jarida la Microbiome la Uingereza
limeonyesha kuwa upigaji busu unaweza kusafirisha zaidi ya bakteria
milioni80 kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Daktari Sophianis Nyomyani wa Hospitali ya Mwananyamala anazungumzia
utafiti huo na kusema bakteria wengi ambao huambukizwa kwa njia ya busu
na wengi huchukulia busu kama njia pekee ya kuonyesha upendo.
Utafiti huo pia umesema wapenzi ambao hupigana mabusu kwa wastani wa
mara tisa kwa siku huwa na bakteria ambao wanaendana na hubadilishana
kila wanapofanya tendo hilo.
“Ni upendo ila kiafya si salama,hata kama wanandoa wanashiriki katika
kupigana busu,isiwe kwa kila mtu,ni lazima kuwe na mipaka,unaweza
kumbusu mtu shavuni,nje ya mdomo,mkononi na kwingineko lakini siyo
lazima mdomoni.