Alo vera ni mmea unaopatikana porini na unafanana sana na mmea wa katani na una miiba pembeni, lakini kuna aina nyingi ya mmea huu isipokuwa hapa nataka kuzungumzia ile alovera ambayo ni chungu.
Mmea huu unasifika kwa kuwa tiba ya maradhi mbalimbali pamoja na uchungu wake, miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na malaria, kuumwa na wadudu, baridi yabisi.
Wataalam wanasema kwamba alo vera pia huleta hamu ya kula na husaidia mmeng'enyo wa chakula tumboni sambamba na kuwasaidia wale wenye matatizo ya shida ya haja ndogo (mkojo) kutoka kwa shida.
Aidha magonjwa mengine ambayo huweza kutibika kwa kutumia alo vera ni pamoja na shinikizo la damu la juu, saratani (cancer) bawasira, mkanda wa jeshi na kusaidia askari wa kulinda mwili.
Pamoja na hayo, Tabibu Mandai anabainisha kuwa alo vera nayo husaidia kuongeza nguvu za kiume na kuwasaidia wale wenye shida ya kuvimba mwilini.
Angalizo: Dawa hii ya alo vera hatakiwi kabisa kutumia mama mjamzito au anayenyonyesha usijaribu kutumia kama upo katika hali hizo tafadhari.