Home
»
AFYA
» TAMBUA KIUNGULIA CHA UJAUZITO NA NAMNA YA KUKIEPUKA
Kiungulia cha ujauzito au HeartBurn kwa kimombo ni miongoni mwa
matatizo yanayowapata wanawake wengi wanapobeba mimba. Kiungulia ni hali
inayopelekea mtu ajihisi kuungua au kuwaka moto sehemu ya katikati mwa
kifua. Tatizo hilo huwapata wajawazito mara nyingi katika miezi mitatu
ya mwisho ya ujauzito, lakini pia wapo wakina mama wajawazito wanaopatwa
na kiungulia miezi ya mwanzoni ya mimba. Ili kuelewa namna ya kuzuia
kiungulia kisitokee ni bora kwanza tufahamu kiungulia kinasababishwa na
nini wakati wa mimba. Kiungulia hutokea wakati kiwambo au valvu
kilichopo kati ya tumbo na umio (esophagus) kinapolegea na kushinda
kuzuia asidi ya tumbo isipenye na kurejea katika umio. Mimba huongeza
kiungulia kwa sababu homoni ya progesterone hulegeza kiwambo hicho.
Hivyo asidi inayozalishwa tumboni hasa baada ya kula hurejea katika umio
na kuleta kiungulia. Kiungulia hutokea katika miezi mitatu ya mwisho ya
mimba kutokana na fuko la uzazi kuwa kubwa na kubana utumbo mdogo na
tumbo. Mbano huo wa tumbo hupelekea vilivyoko tumboni kusukumbwa upande
wa umio au esophagus.
Kwa kawaida kutokula vyakula vyenye
kusababisha asidi na gesi tumboni, hupunguza kiungulia. Vyakula hivyo ni
kama vinywaji vyenye gesi ya carboni, vyakula vyenye kiasi kikubwa cha
asidi kama vile jamii ya maharagwe kama maharagwe, kunde, mbaazi n.k,
nyanya, vyakula vyenye viungo, matunda kama machungwa na juisi ya
machungwa, chocolates, vyakula vyenye mafuta mengi, grape fruit na hata
kitunguu swaumu. Lakini pia inategemea mtu na mtu inabidi ujichunguze na
kuona ni vyakula gani ukila unapata kiungulia na gesi.
Zifuatazo ni njia za kujiepusha na kiungulia:
1.
Kutumia baadhi ya dawa salama zinazozuia kiungulia na gesi wakati wa
ujauzito. Kwa nchi zetu za Afrika Mashariki sote tunaifahamu dawa
iitwayo Magnesium ambayo husaidia kuondoa tatizo hilo. Kama upo nchi
nyinginezo pia natumaiani unaweza kupata dawa hiyo kwa msaada wa daktari
wako. (Muhimu ni kupata ushauri wa daktari utumie dawa gani ya kuondoa
heartburn au kiungulia ambayo ni salama wakati wa ujauzito).
2.
Hakikisha unakula kiasi kidogo cha chakula na usile ukashiba sana. Kwa
kuwa mama mjamzito huwa anasikia njaa mara kwa mara na anahitajia kula
vyema ili aujenge vizuri mwili wake na watoto, basi ni bora chakula
chake ukigawe katika sehemu kadhaa ndogo, na ale mara kadhaa, badala ya
kula sana wakati mmoja. Suala hilo litafanya tumbo lake lisijae na
kusaidia kuzuia asidi isipande juu ya tumbo na kusababisha kiungulia na
gesi.
3. Jitahidi usinywe maji mengi sana baada ya chakula au wakati
wa kula, kwani husaidia kuzalisha asidi tumboni kwa haraka na kuleta
kiungulia.
4. Unaweza kula ubani au chewing gum baada ya kula, kwani ubani kutengeneza mate na mate hupunguza asidi.
5.
Jitahidi usilale tu mara baada ya kula, subiri kama nusu saa hivi ipite
ndio ulale. Unapolala usilaze kichwa moja kwa moja bila mto, bali tumia
mito kuegemeza kichwa ili kuzuia asidi isirejee juu ya tumbo na
kusababisha kiungulia.
Unapohisi kiungulia kunywa glasi ya maziwa au kula mtindi.
Na kama hali hiyo haijatoweka kunywa maji ya moto glasi moja yaliyowekwa kijiko kimoja cha asali.